Saturday, March 21, 2009

Za Kale vs Sasa. Kipengele kipya

Kuanzia wiki ijayo, Changamoto Blog italeta kipengele kipya chenye kueleza na kusikilizisha muziki wa kale kulingana na maisha ya sasa. Pengine kuna changamoto walizoona na ambazo licha ya kuwepo tangu nyakati hizo hakuna aliyezitilia maanani. Pengine walikuwa suluhisho la baadhi ya matatizo ambayo sasa hayapo. Pengine uwepo wao umesaidia kutufikisha hapa tulipo na labda tungekuwa mahala bora ama pabaya zaidi kama wasingekuwepo.
Kuna ukweli wa haya ama mengine mengi?
Tuungane kuanzia wiki ijayo katika Zilipendwa vs Sasa
Asante kwa kuwa nasi wakati wote.
Blessings

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kusema kweli umefikiri jambo zuri sana kwani sio miziki tu ambayo inarudi tena hata mavazi yale tuliovaa wakati tupo wadogo yapo baomba sana miaka hii.

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahahaaaaaaaa. Ni kweli Dada Yasinta. Naona Mavazi nimuachie Master maana yeye anayatambua na kuyamudu vema zaidi.
Mie ntaselebuka na zilipendwa tuu humu changamotoni.
Asante kwa wazo jema

malkiory said...

Heko mzee wa changamoto, kwa nia na dhamira yako ya kutaka kutuletea zilipendwa "Old is gold" sisi vijana wa zamani tunazisubiri kwa hamu.

Yasinta Ngonyani said...

Mzee wa Changamoto, nilikuwa namaana kuwa ni vizuri umeamua kufanya hivyo kwani miziki ya kale au zilipendwa nayo sasa inarudi tena kwani nakumbuka nilipokuwa mdogo mamangu alikuwa anaimba nyimbo na sasa nasisikia tena ziko zinaimbwa kwa hiyo nadhani ni jambo nzuri sana kukumbuka mambo ya mwaka arobain na saba. hayo ya mavazi yalikuwa ni mfano tu yaani sasa hata mavazi ya miaka ya -60 na -70 inarudi kwa hiyo kwanini miziki isirudi? Jumamosi njema kakangu

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Sasa mimi hata sijijui - mzee-kijana, kijana-mzee, kijana-kijana, mzee-mzee, hata sijui lipi ni lipi. Wazo zuri hili mzee wa Changamoto na tunasubiri hii nyongeza mpya katika blogu yako nzuri. Blogu yako ndiyo ilikuwa chachu ya mimi kuanzisha kiblogu changu ambacho pamoja na kubanwa na shughuli nyingi za kikazi na familia naamini kitakuwako kwa muda wote ambao mimi nitakuwako. Lete vitu mzee!