Wednesday, August 25, 2010

CHANGAMOTO YETU BLOG.....MIAKA 2 BAADAE

Ndio, ni miaka 2 iliyopita, tarehe kama ya leo blogu hii ya Changamoto Yetu ndio ilizaliwa rasmi. Katika kufikiria miaka yangu 2 ya kujishughulisha na CHANGAMOTO mbalimbali, na kuangalia zaidi ya posts 690 nilizoweka hapa, najivunia kuona uchaji wa kuandika, uchaji wa kuandikiwa na uchaji wa kuchangia umezidi kuongezeka na kuongeza maarifa kila niandikapo na pia niandikiwapo.
Katika Salaam zangu za kutimiza mwaka mmoja (irejee hapa), nilileta shukrani kwa wengi walioniwezesha kupiga hatua kifikra na kiandishi. Lakini kati ya Aug 25, 2008 na leo, nimejuana na wengi, nimewasiliana na wengi na pia kujifunza mengi toka kwa wengi. Hata nisingeweza kuandika makala juu yao kwani hata orodha ya majina yao ingezidi uwezo wa post.
Mko weengi saana na nawapenda na kuwashukuru kwa kuendelea kunifunza na kunipa CHANGAMOTO mbalimbali.
Binafsi nimshukuru Dada Mariam Yazawa ambaye ndiye alikuwa msomaji wa kwaaanza kabisa kuweka maoni bloguni hapa siku 6 tu tangu kuanzisha blogu. Zaidi yake, nawashukuru nyooote mtembeleao.
Niwakumbushe nilichoandika siku ya kwanza katika BANDIKO LA KWANZA KABISA HAPA BLOGUNI (irejee hapa) ambapo nilisema
"Karibu
Ni mengi ambayo hutokea ulimwenguni ambayo kwa bahati nzuri ama mbaya hatuwezi kujua upande wa pili wayo kwa kuwa hatuwezi kuwa na pande zote kwa wakati mmoja na wala hatuwezi kujua (zaidi ya kuhisi) nini kitatokea ama kingetokea kama tungefanya tofauti na tulivyofanya sasa. Ina maana kuwa maisha ni mapana na yenye mafanikio na maanguko zaidi ya tunavyoweza kufikiria maana hujui kama lile ulilokwepa kulifanya lingekuweka kwenye mafanikio ama maanguko hasa kwa wakati ujao. Nina maana ya kwamba kuna mafanikio yanayopatikana baada ya kupitia majaribio meengi bila kukata tamaa na majaribio wapitiayo wengi waliofanikiwa huwa wanayachukulia kama CHANGAMOTO (challenge) kwao. Nimejifunza kuwa kama kitu hukipendi, basi magumu yake yatakuwa kisingizio cha kuacha ama kutoanza kufanya jambo, na kama wakipenda, basi magumu kwako yatakuwa changamoto kuelekea mafanikio. Tutambue kuwa hatukukimbia kabla ya kutembea na wala hatukutembea kabla ya kutambaa. Hivyo kukaa chini ukaona mafanikio ya walio mbali katika yale upendayo ni CHANGAMOTO kuelekea mafanikio...........
Karibu kwenye "ukanda wa changamoto" (challenge zone) kutoa ama kupokea changamoto mbalimbali."
Miaka miwili baadae, nasema NAJIVUNIA KUWA MMOJA WA WANA-CHANGAMOTO na nakualika katika mwaka mwingine wa kuchangamotoa mambo mbalimbali.
BARAKA KWAKO MSOMAJI

16 comments:

Subi Nukta said...

Hongera Mzee kwa kutimiza miaka miwili ya kublogu. Nakutakia mafanikio mengi zaidi. Upendo, baraka na heshima kwako!

Yasinta Ngonyani said...

Hongera blog ya Chongamoto na pia kaka Mubelwa kwa kutimiza miaka miwili katika ulimwengu huu wa kublog. Na uzidi kuwa na nguvu ili uzidi kutuletea CHANGAMOTO ZAIDI. UPENDO DAIMA.

malkiory said...

Pongezi Mubelwa. Kila la heri na fanaka kwa changamoto zaidi.

emu-three said...

Tunakupa hongera sana kwa kutimiza miaka miwili, na miaka miwili si hapa katika mambo haya ya blog, mengi umeyapitia na wakati mwingine unaweza ukakata tamaa, kuwa uandikacho pengine hakikidhi haja ya wadau, lakini unapangusha macho unaendelea, kwasababu nia yako ni kutoa kile ulicho nacho kwa wenzako. Hongera sana, CHANGAMOTO, tupo pamoja nawe

chib said...

Hongera sana.Si haba, kazi yako tumeiona. Endeleza uzi huu huu

Faith S Hilary said...

Pia baraka kwako "author", hongera nyingi na kamwe sitokoma kutembelea hapa hata kama internet hairuhusu...lol...

John Mwaipopo said...

waliyoyasema wachangiaji walionitangulia ni;
copy and paste! copy and paste!copy and paste! copy and paste!copy and paste! copy and paste!copy and paste! copy and paste!copy and paste! copy and paste!copy and paste!

miaka miwili ya kufunga ndoa ya lazima katika jambo la hiari la kublogu sio mchezo. kuanzia kufikiri nini cha kupost mpaka kupata muda wa kupost sio mchezo

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kazi nzuri na hongera sana!

Simon Kitururu said...

Hongera Mkuu!Hapa ni kibonge ya shule Mkuu!

Albert Kissima said...

Hongera sana kaka Mubelwa kwa kazi zako nzuri. Kwenye baraza lako hili kila kukicha ni changamoto zenye kuchangamsha akili kweli kweli. Kazi uifanyayo si ya kubeza hata kidogo, wastahili hongera kwa hakija.
Kila lenye heri katika mwaka wa tatu na miaka mingine mingi ijayo ya kublog.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ushindi ni lazima!

NAJUA WAJUA said...

HONGERA SANA KWANI MIAKA MIWILI KUWA KATIKA BLOG SI MCHEZO!!

SN said...

Heri ya mwaka mpya Mzee wa Changamoto!! Nilishakwambia kuwa misemo yako na unavyocheza na maneno ni kama "inaibebesha chuma" ubongo wangu! Au yale mambo ya gymnastics!

Hongera sana na upatiwe nguvu na changoto ya kuendelea na juhudi zako!

Koero Mkundi said...

Hongera kaka kwa blog yetu kutimiza umri wa miaka miwili. naamini huu utakuwa ni mwanzo mwingine wa kuendeleza kile kilichopelekea kuanzishwa kwa blog hii....mungu ibariki blog ya chngamoto yetu

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

hongela mkubwa wa kazi!

DIDI VAVA said...

Hongera sana Mkuu Mubelwa na CHANGAMOTO YETU KWA KUTIMIZA MIAKA MIWILI.