Sunday, April 15, 2012

A New Day......Hongera Iddy Sandaly

"..once you got life there's a chance you'll be able to overcome. Where there's will, there's a way, IT'S NOT OVER UNTIL IT'S DONE, if you believe you will achieve, everything can just turn around" Hayo ni maneno yaliyoimbwa naye mkongwe wa Lover Rock Beres Hammond katika wimbo wake Not Over Until It's Done.
Maneno hasa ndio ambayo hunipa moyo pale ninapokuwa na ndoto ama mipango na kisha kuhisi kuwa ninakumbana na vikwazo mbalimbali katika kuyatekeleza. Na ndipo nikumbukapo kuwa It's not over until it's done.
Na ukimsikiliza zaidi kwenye wimbo huo anaendelea kusema kuwa "while you are wondering what suit to wear, the family's worry is what a meal to share" na hiyo hunipa mwanga kuwa pamoja na matatizo tuliyonayo, lakini wengine wana zaidi. Kwa hiyo badala ya kulalamika basi tuendelea kukamilisha mikakati ya kufanikisha ndoto zetu. Na kwa juhudi, maarifa, utii na imani kutakuwa na njia sahihi ya kutufikisha kule tutakako kwenda. Lakini juu ya yote kuwe na Baraka zake akupaye uhai.
Na haya ndio mambo alitokumbana nayo Kaka Iddi Sandaly katika harakati zake za kuukwaa uRais wa Jumuiya ya waTanzania waishio jiji la Washington DC na majimbo ya Maryland na Virginia.
Kwa wiki kadhaa alizopiga kampeni, ameonesha nia halisi ya kushinda uchaguzi huu na mara zote katika harakati zake amekuwa akikumbana na "kigingi" hiki ama kile. Alichofanya ni kuamini katika nia yake ya kuwa kiongozi wa jumuiya na yanaweza kusemwa yasemwayo lakini "it's not over until it's done". Na watu wakasema kuwa historia haiwezi kubadilika kwa mtu ambaye hajawa na uzoefu wa kuhudhuria kila walipo waTanzania kupewa dhamana ya kuongoza jumuiya iliyo kwenye makao makuu ya taifa hili lenye ukubwa wa matatizo zaidi ya wema, lakini msemo unaonekana kuwa uleule kuwa "it's not over until it's done".
Iddi amekuwa na mafanikio makubwa katika "kuiunganisha jamii" tangu akiwa kiongozi wa wanafunzi huko Malaysia na kisha kiongozi wa TAMCO hapa Washington DC. Ni uwezo huohuo alioutumia katika kujipanga na kueleza vema mtazamo, msimamo, imani, changamoto na matarajio yake na namna anavyojipanga kukabiliana na hayo yote katika kipindi cha utawala akipewa dhamana. Alionesha kujipanga vema katika ku-organize kampeni ambayo imempatia dhamana hii
Na leo hii tumeshuhudia akivuka vikwazo vyote na kushinda mchuano mkali na kuchaguliwa kuwa kiongozi
CHANGAMOTO YETU ni kujifunza kutoka katika njia aliyoionesha badala ya kutegemea kuleta mabadiliko Barani na nchini mwetu. Kuamini katika kuvunja mipaka iwekwayo na "wapinzani" na kuamini katika kile sahihi kilichopo ndani ya mioyo yetu.
Ninalohisi ni kuwa "BETTER DAYS ARE COMING."
Hongera sana Rais wa Jumuiya Iddi Sandaly.
Hongera makamu wa Rais Raymond Abraham
Hongera Katibu Mkuu Amos Cherehani
Hongera mweka hazina Genis Malasy.
Hongera wajumbe wetu wa bodi.
Mama Eliserena Kimolo
Ndg. Al Amin Chande
Mama Grace Sebo Mgaza
Ndg. Hamza Mwamoyo
Hongera kwa wote walioshiriki.
Hongera kwa wanajumuiya wote na waTanzania kwa ujumla.
"Better days are coming and i can feel it in the wind. We've been working and praying, and i know by God we'll win....If you believe in him, the miracles will happen...."

1 comment:

Ebou's said...

Hukua kimwili but ulikuwa kiroho pamoja sana kamanda wangu kwa kufikiria upeo wa mbali this is Awesome nani ujumbe tosha