Monday, May 6, 2013

POWER BREAKFAST....Katika hili mmechemsha.

Najua litakalozungumzwa hapa SI JIPYA (kwa maana ya maudhui) lakini ninapenda tuliangalie katika mtazamo wa ki-fani zaidi.
Weka kando kilichozungumzwa katika AUDIO nitakayoweka hapa chini, tuwekeze katika NAMNA KILIVYOZUNGUMZWA.
Katika kipindi hiki (ambacho kimesambaa sana mtandaoni), Bwn. Ruge Mutahaba amefafanua mengi kuhusu kilichompeleka kwenye kipindi hicho.
NA AMEFANYA VEMA
Tatizo linakuja katika kuTAMBUA madhumuni ya kilichorushwa.
Sijasikia mahala popote wakiyataja kama MAHOJIANO (na sina hakika kama mazungumzo haya yana vigezo vya kuitwa hivyo) lakini pia sikusikia yakitajwa kama TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI kwa kuwa pia nina wasiwasi kama yana-fit huko.
Iwapo yangekuwa mahojiano, ningetegemea watangazaji wa kipindi waliosikika kuwa "FAIR & BALANCED" katika maswali yao.
Lakini watangazaji wamesikika kama CHEERLEADERS katika mazungumzo haya "wakijazia" pale ambapo wanaamini "bosi" wao amekosea.
HILI LIMEONDOA SUALA ZIMA LA MAHOJIANO
Na ninapowaza kama nilichosikiliza ni TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI, nawaza kuwa TAARIFA HII ILIKUWA IKITOLEWA NA WATU WANGAPI?
Ukweli ni kuwa watayarishaji na watangazaji wa kipindi cha POWER BREAKFAST wameshindwa kuweka uwiano katika kipindi na wamekuwa zaidi ya cheerleaders kwenye mazungumzo HAYA
Na huu ni mtazamo wangu kwa namna nionavyo tatizo....
Labda NAMNA NIONAVYO TATIZO NDIO TATIZO

1 comment:

Fadhy Mtanga said...

Nakuunga mkono. Nadhani imekuwa mipasho (sijui neno sahihi jingine)
Niulize, tatizo pale ni weledi wa watayarishaji? ama makusudi ya bosi?