Sunday, August 31, 2008

RAMADHAN NJEMA

Mwezi wa Ramadhan umewadia. Ni mwezi wa tisa wa kalenda ya ki-Islam unaoaminika kuwa wa UFUNUO na BARAKA zaidi katika mwaka. Mwezi ambao hujenga imani ya mamilioni ya waaminio kwa KUFUNGA, KUSALI NA KUSOMA KITABU KITAKATIFU na kuadhimisha matukio kadhaa katika kalenda ya dini. Ni kufunga kunakofundisha zaidi juu ya UTU na UVUMILIVU, kusoma maandiko matakatifu na kujiweka kando na matukio ya kidunia, kusahihisha tabia zisizo sahihi, kujitakasa kiroho na kuimarisha uhusiano kati ya mwanadamu na Mwenyezi Mungu kwa kusali, matendo mema,kujitolea kusaidia wasiojiweza na kuchangia ama
kuwawezesha wenye shida mbalimbali.
Naungana na ndugu zangu wote katika mwezi huu mtukufu kuwatakia kila lililo jema katika mfungo na zaidi kuimarisha uhusiano mwema baina yetu wanadamu na Mwenyezi Mungu hata baada ya mfungo kumalizika.
Ramadhan Njema

2 comments:

mumyhery said...

ahsante na wewe pia

Mzee wa Changamoto said...

Asante Mumyhery. Maisha mema popote ulipo