Sunday, September 14, 2008

Mkihama ndo mwaja na mpya?

Mwinjuma Muumin

Kumekuwa na hii tabia ya wasanii wa muziki hasa wa dansi nyumbani kuja na nyimbo mpya kila mara wanapohama bendi na baada ya hapo kufifia kabisa. Haihitaji akili zilizopitiliza kujua kuwa sababu pekee inayopelekea mafanikio yenye "utamu wa bazoka" ambayo hutokea pale msanii anapohama ama kuanzisha bendi ni kwa kuwa nyimbo hizo zitagusia maisha ya alikotoka ambako mara nyingi wanapoingia huwa wanapasifia saana. Ni aina fulani ya majungu ambayo kama mengine huvuma kwa muda mfupi kisha msanii anakuwa "hana nyimbo" tena na kuanza kumtafuta mbaya wake badala ya kukaa na kutafakari mapungufu yao na kutafuta namna m'badala ya kujikwamua na mapungufu hayo. Sasa Mwinjuma anarejea tena akisema AMEFIKA kwenye Bwagamoyo Sound yake , kauli ambayo Mwinjuma sio tu ameshaisema haya mara nyingi, bali ameyaimba katika nyimbo za bendi mbalimbali alizohamia. Si yeye tu, bali wasanii kama Waziri Sonyo, Hussein Jumbe, Ali Choki, Banzastone na wengine maarufu (kwa kuimba na kuhama) wametenda haya pia. Msome Mwinjuma kwenye mahojiano na Edgar Nazar wa MAJIRA hapa www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=siasa&habariNamba=8137

Ushauri wa bure kwa wasanii, "msitamani pepo kabla ya kifo" na wala " msibomoe daraja baada ya kuvuka, mwaweza lihitaji mkirejea"

Ni Changamoto tuu

No comments: