Friday, September 26, 2008

"You eat what you are"

Sangara
Nutrigenomics ni aina mpya ya sayansi ambayo inahusisha uchunguzi wa namna seli zetu za mwili zinavyoweza kuathiri na kuingiliana na tabia yetu ya mlo na ambayo imegundua kuwa genes* zilizo ndani yako ndizo zinazoathiri namna na kiasi unachokula na hata matokeo yake.
Uchunguzi huo ambao bado haujapata baraka zote za wataalamu kutokana na ugumu wa kazi na elimu ya genes hizo na ukweli kuwa mazingira pia huathiri tabia za mlo, umebainisha kuwa waweza kula chakula bora chenye kuzuia kuongezeka mwili na bado ukaongezeka ilhali mwenzio akawa anakula kila kilicho mbele yake na kubaki kama alivyo.
Umeongeza kuwa baadhi ya genes husababisha watu kuathiriwa tofauti na vyakula kama mafuta na protini na pia huwafanya watu wenye nazo kupendelea vyakula vya aina fulani ambavyo kwa namna moja ama nyingine husababisha mwonekano wao kuwa tofauti na wengine. Kwa hiyo wakati tunajitahidi kuamini kuwa tunakuwa tulivyo kwa sababu ya tunavyokula, pia tukumbuke kuwa tunakula tulavyo kulingana na tulivyo navyo ndani mwetu.
Soma zaidi kwa kubofya hapa http://www.arthritis.org/how-genes-influence-your-diet.php

* gene:: a specific sequence of nucleotides in DNA or RNA that is located usually on a chromosome and that is the functional unit of inheritance controlling the transmission and expression of one or more traits by specifying the structure of a particular polypeptide and especially a protein or controlling the function of other genetic material

No comments: