Thursday, September 25, 2008

Nini hasa hutokea wakati wa kufa?

Dr Sam Parnia
Utata wa hisia na nini hutokea ama huendelea katika akili na mwili mtu anayeeleka kufa unaweza kuelekea kupata ufumbuzi baada ya kuanzishwa kwa mchakato wa uchunguzi wa miaka mitatu unaotarajiwa kuhusisha takriban watu 1500 waliokuwa katika hali ya "nusu ufu" (cardiac arrest) kueleza hisia hizo.
Uchunguzi huo utakaoongozwa na mmoja wa wataalamu wanaotambulika duniani kwa uchunguzi wa masuala ya vifo Dr Sam Parnia kutoka Weill Cornell Medical Center iliyoko New York nchini Marekani, akishirikiana na wataalamu wenzake wa mradi aliouasisi na anaouongoza unaojulikana kama Human Consciousness Project utahusisha vituo vikuu vya afya zaidi ya 25 kutoka nchi za Ulaya, Canada na Marekani ukiwa na jina la AWARE na kuchimba zaidi hisia za kibaolojia juu ya kile kilichoitwa "out-of-body experience.
Dr Parnia amehojiwa na jarida la TIME na kueleza mambo mengi yakiwemo utata wa mapingamizi juu ya uchunguzi kama huo, mahojiano yake na mtu wa kwanza kudai kuwa katika hali hiyo, changamoto za kiteknolojia kuhusiana na kile kinachotokea wakati huo na hata njia zitakazotumika kuhakikisha yale yatakayovumbiliwa na uchunguzi huo kwa jamii na waweza kusoma yote kwa kubofya http://www.time.com/time/health/article/0,8599,1842627,00.html. Baadhi ya watu waliosoma habari za uchunguzi wake wameshaanza kujitokeza kuhojiwa ili kuelezea yaliyowasibu ama waliyopitia wakati wa "u-nusu ufu" huo http://answers.yahoo.com/question/index?qid=20080924095843AAYJVP9 .
Pia waweza kupata wasifu wa Dr Parnia kwa kubofya http://www.mindbodysymposium.com/Speakers-Panelists/sam-parnia-md-phd-mrcp.html

1 comment:

Leroy Deo Kimolo said...

KWA UPEO WANGU MDOGO NINAKICHUKULIA KIFO KAMA USINGIZI USIO NA MWISHO AMBAO HUMFANYA MTU KUTOOTA WALA KUTOFIKIRI CHOCHOTE MARA BAADA YA UBONGO KUFIKIA KIWANGO CHA MWISHO CHA UFANYAJI KAZI