Sunday, October 5, 2008

Milo 7 isaidiayo kurefusha maisha.


Kwa miaka nenda rudi, wanasayansi wamekuwa wakizunguka dunia kutafuta jamii ambazo zimesemekana kuwa na maisha marefu na yenye afya njema ili kuweza kufichua siri ziwafanyazo waishi maisha muda mrefu namna hiyo. Katika miongo michache iliyopita wameweza kupata machache yenye kutia moyo juu ya hilo. Kwa mujibu wa jarida la Eating Well, wachunguzi wanasema kutumia Olive Oil kumewasaidia Wagiriki kupambana na maradhi ya moyo wakati vyakula vyenye kiasi kikubwa cha samaki kimesaidia wazawa wa Alaska kupambana na matatizo ya mishipa ya moyo. Pia siri ya maisha marefu katika visiwa vya San Blas ufukweni mwa Panama imetambulika kuwa ni matumizi ya chocolate ambayo imeonekana kusaidia kuweka mishipa ya damu katika hali ya afya njema. Huko kusini mwa Japan katika kisiwa cha Okinawa ambapo wakazi wake wanaotimiza miaka 100 wanabashiriwa kuwa mara tano ya nchi zilizoendelea ( watu 50 kati ya 100,000 wana zaidi ya miaka 100 ukilinganisha na 10 walioko Marekani na nchi zilizoendelea) na siri ya kuishi kwao maisha marefu ya afya ni Viazi vitamu, matunda yajulikanayo kama Bitter Lemon na Chai ya Sanpin (ambayo ni mchanganyiko wa green tea na maua ya Jasmine) na vyote vitatu kwa pamoja vina virutubisho vinavyosaidia kuziua kulika kwa cell za mwili.
Unaweza kujua zaidi juu ya milo 7 inayoweza kusaidia kurefusha maisha kwa kubofya http://www.eatingwell.com/recipes/collections/7_foods_to_keep_young.html

No comments: