Innocent Galinoma
"tell the children the truth right now, right now; what's going on with their economy, rain is falling but there's no food why, where is justice, where is equality, why there is murder, poverty and blood everywhere, where is education, medication for my children?......tell me the truth right now" ni maneno toka kwake Innocent Galinoma Mfalingundi anapomalizia wimbo wake Africans. Kila mara ninaposikiliza kibao hiki (ambacho nimekisikiliza mara nyingi saana) najiuliza maswali mengi ambayo yameanzishwa na msanii ambaye ninaheshimu kazi zake kutokana na ujumbe wake na uwakilishaji wake (kuanzia lugha mpaka midundo kulingana na mahadhi atumiayo).Africans ni moja kati ya nyimbo ambazo ujumbe wake ni m'bichi leo kama ulivyokuwa wakati unatoka mwanzoni mwa miaka ya tisini. Katika kibao hiki, Inno anauliza mengi kuhusu Afrika na waAfrika akitukumbusha juu ya Upendo, Jasho na hata nguvu kazi zinazowekezwa barani kwa tumaini la kupata matokeo mema, lakini bado kinachojionesha dhahiri ni uasi na kukandamizwa kwa waafrika na kibaya zaidi vikifanywa na WaAfrika wenzetu ("..only this time the downpressor man Yeah!!, happens to be my own brother..")
Ni yale ayaonayo ambayo ameyaweka wazi katika wimbo huu yanayonifanya nishangae kama wale wenye mamlaka na madaraka wanatambua maswali ambayo wanapaswa kujibu kwa watoto wa Afrika ambao wanakabiliwa na matatizo haya sugu yasiyoonekana kuwa na mwelekeo ama tumaini la kutokomea ndani ya kizazi chao huku waheshimiwa hao wakiendesha na kuishi maisha mwanana. Ni hao hao ninaoamini anawashangaa kwa kuwakandamiza waAfrika wenzao na kujitengenezea maisha mazuri kwa mgongo wao. Swali kubwa analouliza Inno ni kwamba kwanini tusiishi kama Mungu alivyopenda tuwe? Tumekuwa watu wa visingizio vya kuwepo kwa rushwa, umaskini na mauaji kila mahali lakini ukweli utabaki kuwa tunashindwa kujiuliza twaelekea wapi. Anahimiza namna Mungu alivyotaka tuishi kwa "One Love, One Aim , One Destiny for everyone"
Inno Galinoma ni kati ya wasanii wenye uwezo mkubwa saana wa kuwakilisha ujumbe-mkombozi kwa watu wa rika, imani, itikadi na asili mbalimbali kwa kutumia muziki anaoumudu vema. Kazi zake kama Kilimbanjaro ama Running zaweza kuwa kithibitisho kingine cha namna anavyoweza kuiweka jamii katika taswira halisi ya kile azungumzacho kiasi cha mtu kujihisi unaona liimbwalo.
HESHIMA KWAKO INNO NA SASA NI CHANGAMOTO YETU KUTEKELEZA YALE UTUELIMISHAYO.
Blessings
Picha hisani ya www.bongoland2.blogspot.comBofya hii player hapa chini usikie kipaji cha Inno kwenye kuwakilisha jamii**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.IJUMAA NJEMA
No comments:
Post a Comment