Wednesday, October 22, 2008

Remembering Maestro Ndala Kasheba


Kama kuna wasanii waliojijengea heshima kwa kutunga, kuimba na kucharaza vema ala za muziki, basi miongoni mwao ni Ndala Kasheba. Mtunzi na mwanamuziki huyu mahiri aliyepewa jina la Maestro kutokana na kazi zake alikuwa msanii mwenye uwezo mkubwa sana wa kutunga nyimbo zenye kugusa matukio halisi yaikumbayo jamii ha hata wakati mwingine yaliyomkuta yeye binafsi.
Tunakumbuka nyimbo kama Kesi ya Khanga na hata Yellow Card ambazo sio tu zilipata umaarufu kwa umahiri wa mpangilio wa muziki, lakini pia aliezea mikasa halisi ya maisha jambo ambalo linaendelea kuwa funzo kwa wengi.
Kasheba ni kati ya wakongwe wachache waliotutoka miaka kadhaa, na leo tunapotimiza miaka minne tangu atangulie tuelekeako, bado tunajiuliza nani wajao kuendeleza kazi za wakongwe mahiri kama hawa. Sanaa ya muziki inazidi kupungua umuhimu wa uwakilishaji wa jamii kama ilivyokuwa enzi za kina Kasheba na wasanii wanajali zaidi hisia binafsi na kurandanisha majina badala ya kufumbua mengi yahitajiwayo kufanya hivyo huko vijijini na sehemu nyingine.
Ulitenda kazi yako Vema Ndala, na leo tunapotimiza miaka minne tangu ututoke, tunakumbuka na kuheshimu kazi zako na tunaendelea sio tu kufurahia kazizo, bali kujifunza yale yaliyoimbwa katika nyimbo zako.

Pumzika kwa Amani NDALA MAESTRO KASHEBA

1 comment:

ARUSHA SEKII ALUMNI said...

Asante sana kaka kwa kutukumbusha Mkongwe marehe kasheba, nakubaliana kabisa na yote uliyosema hukuk nikibaki na majonzi kuhusu hatima ya mkongwe mwingine Mzee Nguza au babu Sea.unaweza kunitembelea pia katika www.yangoyo.blogspot.com na ninakutakia heri ya mwaka mpya