"Do you ever worryAbout leaving home and Coming back in a coffin, With a bullet through your head. So join us and fight this Crime and Corruption"
Hayo ni maneno ambayo ni kama yalitabiri mauti yake mwenyewe miaka 8 kabla hayajamkuta. Ni kutoka katika wimbo wa Crime and Corruption uliko kwenye albamu ya The Way It Is na ambacho pengine ndicho kilichotokea kuwa maarufu na kutiliwa umakini na walimwengu wengi mara baada ya kifo chake. Sababu kuwa ni namna alivyoeleza matukio yanayomsikitisha na kuendelea kufumbiwa macho na viongozi jamiini mwake. Lucky amewalilia viongozi kuacha kupuuzia hali halisi ya Rushwa na Maovu katika jamii yake na kukutana na wahanga wa matatizo hayo jambo ambalo aliamini labda lingefungua mioyo ya viongozi na kuendeleza kampeni za kupinga mambo hayo. Ukiusikiliza kwa makini, Lucky alianza na swali kwa "waheshimiwa" akitaka kujua sababu hasa inayowafanya wasione ukweli juu ya wakulima na askari wanaouawa kila siku huku wao (viongozi) wakitoa ripoti kuwa hali si mbaya na anawauliza " Is it the bodyguards around you,Is it the high walls where you live,Or is it the men with the guns around you twenty four hours a day;That make you ignore the crying of the people..."
Ni ukweli ambao aliuimba na kwa bahati mbaya saana ndiyo yaliyomkuta miaka minane baadae pale alipouawa katika aina ya uovu ambao si mgeni na umekuwa ukikemewa saana nchini Afrika Kusini. Aliimba katika kibao hiki juu ya wizi wa magari uliokithiri ambao wakati mwingine unafanyika mchana kweupe tena kwenye barabara kubwa kama Highway 54. Hiyo ni hali halisi ambayo hata baadhi (wengi) ya watu walioihama Afrika kusini wanasema wamekimbia maovu kama hayo na hata Kampuni ka bima ya Hollard Insurance iliamua kutowekea bima magari ya Volkswagen Citi Golf kutokana na kuibiwa sana nchini humo (bofya http://en.wikipedia.org/wiki/Crime_in_South_Africa). Lakini kama askari halisi wa Reggae na ambaye alikuwa mstari wa mbele kutetea wanyonge, Lucky Dube aliweza kuimba haya na mengine mengi katika Albamu yake hii ya The Way It Is ambayo viongozi wengi waliamua na bado wapo wanaofumbia macho huku uovu huu ukiendelea kuziathiri jamii zetu barani Afrika na Duniani kwa ujumla.
RUSHWA na MAOVU ni kati ya mambo aliyoyapigania saana Lucky Dube, na leo ikiwa ni siku moja pungufu ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu auawe, CHANGAMOTO YETU ni kuangalia namna ambavyo mengi mema yaliyoimbwa naye yanatafutiwa ufumbuzi katika jamii zetu. Video ya sehemu ya mazishi yake na heshima kwa Lucky ni hii hapa chini
Blessings
**Them, I & Them ni kipengele kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
No comments:
Post a Comment