Thursday, October 30, 2008

Uchaguzi wa Vijana CCM Wilaya ya Misenyi

Kamanda wa vijana na CCM wilayani Misenyi Protace Ishengoma akiteta jambo na Katibu wa CCm wilayani Misenyi Joseph Kagashe muda mfupi la kufungua mkutanio wa kuwachagua viongozi mbalimbali wa UVCCM wa wilaya ya Misenyi.
Mwenyekiti wa CCM wilayani misenyi Paul Mgomba akifurahia jambo na kamanda wa vijana wa CCM wilayani Misenyi Protace Ishengoma baada ya kufungua mkutano wa uchaguzi.
Habari na picha toka kwa Audax Mutiganzi na Mukebezi Rugarabamu. Misenyi Kagera
Kwa niaba ya wanaChangamoto wote, nawatakia mafanikio mema katika kuanzisha na kuendeleza mema mengi kwa manufaa ya jamii nzima.
Mzee wa Changamoto

3 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

aisee mbona kamanda wa vijana na mzee kiasi hicho? inabidi vijana waamie wanakotakiwa bwana vinginevyo hawana sehem ya ku-pray

Mzee wa Changamoto said...

That's right KJL. Ujumbe utakuwa umefika. Ila sina hakika na mwisho wa ujana ni upi. Na sina hakika na miaka ya "kijana" huyu. Ama Kamanda anaweza kuwa mzee? Maana si tunawaona kina Kingunge na Lowassa kwenye UVCCM? Ila nadhani si ma-kamanda wale.
Blessings Kamala

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hapo sasa. ujana unaeleweka muda wake na wakati wake. lazima ngozi iwe inang'ra bado, nguvu lukuki na lugha kibao za kileo.
ujana ni wakati ambapo akili inafanya kazi kwa kasi etc. inaeleweka mwisho wa ujana. huwezikumwita mtu wa over40 kuwa ni kijana, huo ni upofu. kijana lazima awe yanki kiumri.
je ni wazee wangapi unawaona waki-blog?
akina Lowasa, Kingunge etc kuwa kwenye UVCCM, maanake CCM inawatambua wazee AKA vijana wa zamani na ndio maana vijana makini wanaamia vyama vya upinzani.