Friday, January 7, 2011

Them, I & Them. INNOCENT GALINOMA ......... Kilimanjaro

"i see government people downpressing their own people,..."
"Standing on the mountain top, of mount Kilimanjaro, the highest mountain in Africa, there i see illussions....I see children are crying, i see children dying, i dont see children playing, children don't have no fun. No education for children, no medication for them" ......" i don't see peace nowhere, no sign of love anywhere now..."
Kwa mara ya tena ni msanii niaminiye kuwa mmoja katu ya wasanii bora zaidi katika uwakilishaji wa ujumbe kupitia muziki wa reggae hapa ulimwenguni, Innocent Galinoma Mfalingundi aliyeimba haya kwenye wimbo wake wa Kilimanjaro. Akitupa taswira ya yale yanayoendelea katika Bara letu la Afrika.
Ni haya aliyoimba Inno kwenye wimbo wake huu ambayo tunayaona yakiendelea kujitokeza katika maisha ya waAfrika wengi takribani miaka 18 tangu atoe kibao chake hicho. Na aliyoyaona kipindi hicho ndiyo yanayoendelea kutokea hata sasa. Kwenye wimbo wake alisema "i see government people downpressing their own people" Photo Credits: WAVUTI.COM
Na hilo ndilo tunaloliona. Tumeona namna ambavyo haki ya wananchi kwa serikali imekuwa kama ni NA SI HAKI. Kuwa kwa kile kinachoitwa kulinda maisha ya wananchi tunashuhudia hao hao wananchi (kwa makusudi ama bahati mbaya) wakiuawa na wale wenye dhamana ya kutunza uhai na usalama wao. Tumeshuhudia haya hata siku kadhaa zilizopita huko Arusha. Ni kama walio juu wamejisahau vile na ndio maana humohumo kwenye Kilimanjaro Inno akaendelea akaendelea kuwaonya walio madarakani kuwa "people you meet on your way up, you gonna meet them on your way down"Kujisahau kwa viongozi wengi na kudhani wataendelea kuwa juu milele ndiko kulikotufanya tushuhudie transitions ya HEROS TO ZEROS toka kwa Mamilionea walioishia kumalizia maisha yao kwa namna ya kusikitisha kama kina Hayati Mobutu ama Saddam Hussein ambao licha ya kusadikika kuwa na mabilioni ya fedha walilazimika kuishi maisha ya kusikitisha na fedheha katika siku za mwisho za maisha yao.
Lakini pia Inno haachii kwa kueleza hayo aonayo na aaminiyo kwa viongozi, bali pia anaeleza wale wanaoteseka kuwa watayashinda kama walivyoshinda wale walioandikwa kwenye vitabu vitakatifu anaposema "yet i know we shall survive; like Shadrack, Meshack and Abednego, thrown in the fire, but never get burn"
Nini waweza tegemea kuona kama ukisimama juu ya mlima Kilimanjaro na kuitazama Afrika ama Tanzania? Kitu kilichobadilika kwa nionavyo mimi ni RAHA kwa waliokwangua mali za umma kifisadi na KARAHA kwa wenye kuendelea kutenda yaliyo haki wakiendelea kukwanguliwa na wachache. Bofya Player usikilize ujuzi wa ajabu alionao Inno kuelezea matatizo halisi ya Africa.

NIMESEMA NIONAVYO MIMI NA AMINI USIAMINI YAWEZEKANA NAMNA NIONAVYO NDILO TATIZO
BLESSINGS
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

9 comments:

Rama Msangi said...

kamanda, wapi kitabu ya wageni kwa ajili ya sisi tunaopita kujiandikisha? Well, ni msangimdogo hapa, ambaye Bwaya, anasema nimepotea, ila ukweli ni kuwa nipo. Maskani yangu kwa sasa inaitwa: www.uchambuzi.blogspot.com/. Nakukaribisha wewe na wadau wenzako huko maskani kwangu na kuna kitabu cha wageni mtajiandikisha:

kwa mawasiliano binafsi, niandikie: msangirs@yahoo.co.uk au @gmail.com

Subi Nukta said...

Siku ukibahatika kuupata wimbo wenye mashairi, 'standing on the mountain top' tafadhali naomba nigawie. Nimeutafuta sana huo wimbo sijaupata na sina namna ya kuwasiliana na Inno nimwombe wimbo wenyewe.

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Msangi. Ni zaidi ya heshima na furaha kuwa nawe hasa siku kama ya leo ambapo kwa kutumia kazi za wasanii, tunaoanisha harakati zao na hali halisi ya changamoto zitukabilizo huko kwetu. Karibu nami natoka kuelekea kwako (nikimalizana na Subi). Da Subi wimbo wenyewe ndio huo huo uusakao. Nilikuwa sijaweka player lakini sasa ndio hiyo hapo.
Jinome, usome hayo, uangalie hali halisi ilivyo Afrika kisha "jiweke" mlimani kuangalia unaona nini.
Inno namheshimu kwa kazi zake na mara kadhaa tulizozungumza tukiwa nyumbani nilijenga heshima kubwa saana kwa mtazamo wake wa kazi za sanaa na maisha kwa ujumla.
Enjoy

Subi Nukta said...

Huu ndiyo wimbo wa kusililiza! Asubuhi.Mchana.Jioni
Watoto.Vijana.Wazee
Huu ni wimbo wa kusikiliza!
Hakuna siku nimefurahi kama leo ukizingatia nimekuwa nikiutafuta tokea mwaka 2006! ndiyo 2006 Disemba!
Whew.... my day has been a mwaaaah!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ni wimbo mzuri wa kiharakati! Na kwangu mimi binadamu daima ataendelea kunishangaza mathalani kwa haya yaliyotokea Arusha. Heri asomaye alama za nyakati na kuiheshimu historia.

Bwana Msangi - Huko uchambuzi blogu mbona nimekutana na mabandiko ya zamani tu - 23/8/2010? Au nimepotea njia? Kama ni hivi basi pengine nami niungane na Bwaya kudai kwamba umepotea ingawa unadai kwamba eti upo!

Da Subi - popote ulipo, heri ya Mwaka Mpya kwako na familia yako!!!

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Matondo. Ni kweli kuwa huu ni UANAHARAKATI wa hali ya juu.
Kuhusu Kaka Msangi ni kuwa alibadili JUKWAA. Sasa hivi anapatikana http://www.jukwaahuru.com/ ambapo ndipo anapoendeleza u-JUKWAA HURU
BLESSINGS

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Galinoma siku hizi anajinoma wapi?
Wimbo wake ni wa kifalsafa ingawa bahati mbaya haukutangazwa na media za nyumbani

Subi Nukta said...

Kaka, Prof. Matondo, asante kwa salam. Heri kwa sikukuu ya Mwaka Mpya nawe pia. Sasa mapumziko yangu yanaanza rasmi! Tutaonana tena kwa wingi kuanzia mwishoni mwa mwezi ujao!
Mbarikiwe ninyi nyote!

nyahbingi worrior. said...

mmmmmmmm ndio mwanzo nasio mwisho mkuu.