Friday, January 14, 2011

Tafakari ya leo

Labda UNYOOFU si suluhisho la kutufikisha kila tunakotaka kwenda, japo twatumia unyoofu kama kielelezo cha kuelekea mafanikioni.Labda waTanzania tu-wanyoofu saana ilhali Tanzania yetu imeshapinda. Ndio maana ni kama twaendesha ki-ajali ajali
Labda Rais Kikwete yu-mnyoofu ilhali serikali na Tanzania yake imepinda. Ina maana hatatufikisha
Labda twajitahidi kuwaza ki-nyoofu ilhali suluhisho la mawazo hayo tayari limepinda. Ndio maana matokeo ni kutofika tutakako
LABDA HATUWAZI KULINGANA NA MAZINGIRA NA LABDA ILI TUSONGE MBELE, TWAHITAJI DEREVA ANAYEONA BARABARA IMEPINDA NAYE AKAPINDA KULINGANA NA BARABARA HIYO ILI TUFIKE TUENDAPO.

NAWAZA KWA SAUTI TU

2 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kezilahabi anaieleza safari yetu ya kuendea nchi ya ahadi kama ifuatavyo:

“Mtakwenda! Halafu mtapinda, mtapinda tena, halafu tena mtapinda, mwishowe mtapindapinda hadi mtakapofika mabonde yenye matope. Mtapita katikati ya matope. Halafu milima, halafu misitu yenye miiba hadi mtakapofika jangwani. Kutoka jangwani mtaingia tena bondeni chini kwa chini hadi baharini. Hakuna mitumbwi wala ngalawa. Mtaogelea, ingawa kuna papa wengi. Mkishavuka mtafika nchi iitwayo Svoboda. Kabla ya kuondoka katika nchi hii itawabidi kupambana na majitu yanayofanana na mimi. Mkitoka hapo mtafika kwenye njia nyembamba. (Akiwaonyesha mawaziri) Hawa hawatapita hawa! Njia hiyo itawafikisha katika nchi iitwayo Fraternite. Kutoka Fraternite mtafika Usawa. Ulizeni tu watu watawaonyesha! Mkifika Usawa mtawakuta Waswahili wenzenu wameketi nje ya ikulu ndogo ya Ravensto” Kaptula la Marx (uk). 20)

Kwa habari zaidi soma hapa:

http://matondo.blogspot.com/2010/01/euphrase-kezilahabi-kaptula-la-marx-na.html

Pole kwa kupotea kwa wiki moja na ushee hivi na afadhali umeibuka tena. Inaonekana masomo yamekukaba kwelikweli. Safi sana!!!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Na tukifikiria vizuri, kama viongozi wetu wamepinda mimi nadhani hata sisi waongozwaji tumepinda pia. Ati, mbona tunakubali kupelekwa ndiko-siko? Kwa nini tunakubali kupelekwa tusikotaka?

Au ni yale yale ya kisa cha Waisraeli walioishia kuzunguka jangwani kwa miaka 40 wakimfuata kiongozi aliyekuwa akiwapindishapindisha!