Wednesday, November 26, 2008

What if we "what ifs" positively?

Pengine swali la kwanza ni "What if Mubelwa angeandika heading hii kwa kiswahili?'
Na ningejibu kuwa yawezekana usingevutiwa nayo, ama isingeweza kuleta maana nitakayo, labda usingethubutu hata kusoma maana yawezekana umeshtushwa na kichwa hiki cha habari u labda unasoma maana unataka kuelewa yamaanisha nini kwa kuwa ni kama haieleweki.
SAFI.
Ndilo lengo kukufanya usome maana ukiangalia uwezekano wa maswali mengi, utagundua kuwa yatakuwa ni "negatives" zaidi.
Lakini hapa lengo si kueleza sababu ya kichwa cha habari. Hapa nataka kuuliza mawili matatu juu ya hali halisi ya utata ambayo imekuwa ikituyumbisha katika maisha yetu. Ni ile hali ya kuogopa na kuhisi kitu kisicho cha mafanikio kitatokea katika kile ambacho mtu anataka kufanya.
Kuwa na ile hali ya kutanguliza kushindwa katika mipango mipya na ni hali hiyo ambayo inatukatisha tamaa na kutukwamisha wengi.
 Kuna mtu aliniambia "your mental picture will determine your actual future" na ni katika hili tunapojijengea maanguko kwenye mipango yetu mipya kwa kuuliza "what if" isipofanikiwa? Labda tujiulize ni mara ngapi tumetaka kufanya kitu kisha tukaamua kuacha kwa kuambiwa hatutafanikisha ama kujiambia wenyewe "itakuwaje nisipofanikisha?" Tusilojua ni kuwa kwa kutofanya ama kuanza kufanya vitu hatutakutana na CHANGAMOTO zilizo muhimu katika kukua, kukomaa, kupevuka na kuendelea kwetu.
Ina maana kwa kutofanya yale tupendayo tukihofia kutofanikiwa tunajifungia milango ya kuendelea kwenye maisha yetu na hilo linafanya wengi wasiopenda kujaribu ama wanaoshindwa kujaribu kwa kuhofia majibu mabaya ya "what if?' kushindwa kutimiza ndoto zao kwa kufanya kazi wasizo na mwito nazo, jambo linalowafanya wakose ubunifu unaostahili na kisha kuifanya kazi kutokuwa ya furaha kama ambavyo ingestahili.
Hili linayafanya matokeo ya kazi kutokuwa katika kiwango kinachotakiwa na kusababisha jamii kutopata "matunda" halisi ya kazi hizo.
Natambua kuwa jamii ingenufaika kama kila mtu angeweza kufanya kile apendacho na ni rahisi kufanya hivyo tukiacha kukatishana tamaa kwa kutilia mkazo na kuulizana "matokeo hasi" (negative results) za kile tutakacho kufanya. Mtambuzi Shabani Kaluse aliwahi kuzungumzia juu ya hofu ya kesho kuwa kama dubwana la kutisha
Sasa naamini twatambua kuwa kuna maswali ya kujiuliza katika harakati zetu za kuikwamua jamii na langu ni "what if we 'what ifs' positively"? Nadhani itasaidia kuwafanya watu waamini katika ndoto zao na kufanikisha mengi kwenye jamii.
Ni mtazamo tu

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza nashukuru sana kwa makala(mjadala ) huu. Hili jambo lilikuwa linanikera sana. Hii ni kweli watu hukatishana sana tamaa kwani mara nyingi watu wanasema usifanye hivyo kwani hapatakuwa na mafanikio. Je wao wanajuaje bila kujaribu?. Na sio katika jamii tu hata katika makazi yaani ofisini nk. ukitoa maoni au ukija na swala fulani yaani kama kufanya mabadiliko nk.utasikia haiwezekana kwani hatuwezi. iwe hivyo hivyo je mmejaribu hapana. Lakini iweje mkate tamaa kabla hujajalibu? Katika jamii hii ya kutiana moyo bado sijaelewa itakuwaje nimtie moyo ndugu yangu ambaye hataki kuwa padre yaani hana wito au ndoto ya kuwa padre je ni busara kumtia moyo?
ni mawazo yangu tu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mzee wa changamoto. rangi za blog yako zinanichanganya macho bwana. yaani nyeusii kwa nyeupe duh? siwi negative but think about it. yaani nikisoma macho yagombaaa.

kwenye negative kunaanzia mbali. hata kwenye nyumba za ibada tunaambiwa jinsi tulivyokuwa nauwezekano wa kuingia motoni zaidi ya rahani. kwa hiyo hii yaanzia mbali ngugu