Thursday, January 1, 2009

2009. KUMEKUCHA

"Kumekucha jua lachomoza asubuhi na mapema. Jumatatu, Jumanne, Jumatano wiki, mwezi mwaka. Siku zenda mbele, zikisonga mbele hazirudi nyuma." Ndivyo walivyoanza wana Twanga Pepeta katika wimbo wao waliouita KUMEKUCHA ambao ni kati ya nyimbo zao za awali. Ujumbe mwingi na midundo ya kufikirisha. Naye Banza alipokea sehemu yake kwa kusema "unapotaka kuanza maisha anza sasa, usisubiri kesho, kesho sio yako, utamkuta mwana si wako."
Ni mwanzo wa mwaka na nataka kutosubiri kesho kukumbushana kuhusu hili. Ni vema kuanza mikakati yote ya mwaka sasa, hata kama si kwa kiwango utakacho. Pale mambo yatakapokuwezesha kuwa utakavyo kwa kiwango utakacho basi utafanya utakavyo. Anza kwa "haba na haba" maana si muda "utajaza kibaba". Biashara asubuhi, shauri yako.

Wasikilize wana Twanga Pepeta kwa kubofya player hiyo hapo chini.

Wimbo kwa hisani ya East African Tube ambayo waweza kuitembelea kwa kubofya hapa

No comments: