Wednesday, December 31, 2008

Happy New Year Bloggers

Amani Heshima na Upendo kwenu waungwana.
Mwaka 2008 waelekea kumalizika na kwa hakika umekuwa na mengi ya kusimulia kama ilivyokuwa kwa miaka mingine. Lakini pia naweza sema ninawasiliana nanyi kama "blogger" mwenzenu ambaye nimejiunga na ulimwengu huu mwaka huu. Kwa hiyo kwangu hilo ni jambo jingine la kukumbuka. Nakumbuka mwaka jana niliponunua kamera yangu kwa msaada wa Brother Michuzi niliendela na ka-ulevi kangu ka libeneke la taswira na kaka Issa akanishauri kuanzisha blog. Kwangu lilikuwa jambo jipya maana sikuwahi kuwa nalo mawazoni mwangu hata nukta moja ya maisha yangu. Nikafikiria na kugundua kuwa kwa jamii ya kiTanzania, ule muda wa ku-blog kwa kiingereza umepita na sasa ni swahili time kwa wanahabari wa blogu. Nikaanza kusoma na kupitia blogs nyingi kujua nini chakosekana. Nikakuta kuna mengi ya maana humo kutuwezesha tujielewe tunavyoishi na ni utambuzi na kujitambua huko kunakotuwezesha sisi ama mwananchi mimi kujua litokealo ulimwenguni. Kwenye blogs hizi twaweza kusoma kali na mpya toka bongo iwe ni kwa ziara na maonesho ya Celebrity wa kigeni ama bongo celebrity. Sikwaziki na ulimwengu kwani nijisikiapo natazama nyimbo za dini ama kutembelea blog maalum iandikayo Injili tupu (yaani strictly gospel) Wapo pia wajiachiao na bambataa. Ni hapa kwetu (kwenye blogs) ambapo hunifanya nijiachie kimawazo tena yasiyo ya kitoto ambayo lengo lake ni kuisaidia jamii ijikomboe kupitia nyanja mbalimbali kama ujasiriamali / saikolojia. Ni hapa kwetu patufanyapo tupate chakula ya mawazo (yaani food for thought) na kisha kusoma mengi yenye kutuwezesha harakati zetu kuanzia pilika za chekechea mpaka pilika vyuo vikuu. Tunawezeshana katika mambo mbalimbali kama taarifa juu ya scholarships na mengine mwngi yahusuyo shule. Ni kweli kuwa si blogs zote ni za kutafakarisha na si blog zote zaandika mengi kama haya, na ni kwa sababu si wakati wote na wala si watu wote twahitaji kusoma na kufikiri. Twatakiwa kujikita pia kwenye spoti na starehe, kuwa na full shangwe kwenye nyanja mbalimbali kuanzia collections, fashions na absolutely awesome things nyinginezo.
Mwaka huu pia umeshuhudia kuvumbuliwa kwa mengi na ni udadisi na uchambuzi wa kalamu za blogs hizi uanikao uozo mwingi ambao wakati mwingine umemfanya mwandishi aonekane mpayukaji lakini pia umejenga hofu. Twawaona viongozi na hofu ya kalamu zetu na hata hofu ya kamera zioneshazo picha mbalimbali za nje na hata bongo pix na kufunua ukweli ujitokezao kuanzia vijijini kwa kina Mwenyekiti Mjengwa mpaka kijiweni. Kwenye mabaraza pia. Kotekote blogs zawakilisha na kwa hakika nia yaonesha kuwa njema na kwa mwendo huu, basi wenye kuburudika wataburudika, wenye kuelimika wataelimika na wenye kusaka mema wasakayo watapata maana blogs ni nyingi na ukiwa na muda basi utaona na kusoma upendacho. Tumejenga udugu wa hiari na sasa najua popote naweza kutembelea. Nimepata karibu toka sehemu zote za nchi toka kwa Dada wa Vukani mpaka Karibu Nyasa. Na tukikutana ni kuendeleza lengo la ku-blog ambalo ni Kuelimisha, kuburudisha na kuikomboa jamii na kwa mwongezeko wa ufanisi na umakini kwenye nyanja hii, naamini tutafika tu.
Kasi ya ukuaji wa uhabarishaji katika fani mbalimbali unazidi kukua na kila siku aja mpya na kama Beres Hammond alivyosema kuwa "just when you think you've seen it all and know it all, suprise suprise suprise, here comes another suprise" nami naamini kuna wajao wenye umakini zaidi wa kugusa matatizo na kuleta suluhisho zaidi kwa jamii yetu na kwa kuwa nia ni njema, na kwa kuwa hatuna nia ya kukata tamaa, basi naungana na Beres akisema "it's not over until it's done"
Nasindikiza salamu naye Robert Nesta Marley akisema KEEP ON MOVING ambaye anasema kuendeleza libeneke licha ya yale akabilianayo nayo. Let's all "keep on moving"

18 comments:

Koero Mkundi said...

Kaka ubunifu ulionao unapaswa utoe albam yako ya bongo fleza,
Maana umenishushia mashairi si mchezo!!!
kaka hicho ni kipaji, usikikalie.
Blessing man.

Fadhy Mtanga said...

Kaka Mubelwa, mzee wa changamoto, nakushukuru sana kwa post yako ambayo umeiandika kwa ufundi mkubwa mno. Nimeipenda sana.
Pia naomba kutumia fursa hii kukutakia kheri katika Mwaka Mpya.
Pia wanablog wote.
Wasomaji wetu.
Watanzania wote kokote waliko ulimwenguni.
Mungu atubariki sote.

Mzee wa Changamoto said...

Shukrani sana Dada Koero na Kaka Fadhy. Ni uwepo wenu na wa wadau wa blogs kama ninyi unipao nguvu na uelewa pia. Nimejifunza mengi sana katika blogs hizi na kwa hakika najivunia kutambuana nanyi. Mmekuwa zaidi ya bloggers wenzangu na nimeona jinsi huduma ama kazi ama blogging inavyoweza kuleta raha na kukuza undugu wa hiari. Nawapenda na Nawaheshimu sana.
Blessings

Subi Nukta said...

...na katika kusoma blogu zote, ndipo ukagundua kuwa changamoto yetu" iwe "The Way You See The Problem Is The Problem".
Heri ya mwaka bloga, Mzee wa Changamoto.

Mzee wa Changamoto said...

Subi, nimechoka kusema juu yako na najua sitaweza kusema enough. Kwa hiyo ubarikiwe tuuu huko uliko. Kilicho cha ajabu ni kila mtu alivyo muhimu ulimwenguni humu. Namaanisha ila mtu kulingana na namna upatavyo NEEMA toka kwao. Siwezi ku-grade ndugu zangu nyie, ila kila mmoja kwa nafasi yake ni SPECIAL. You're all my heroes.

Christian Bwaya said...

Kaka kazi njema sana. Kufanya ubinifu huu, unahitaji akili za ziada. Hongera kwa hilo.

Kwa mwaka huu unaoanza, ili tufanikiwe nadhani, tunahitaji kufanya kitu kimoja tu; kuelewa kuwa tatizo si tatizo lenyewe, tatizo ni sisi wenyewe. Tubadili mitizamo yetu (attitudes). Mafanikio ni halali yetu.

Kila la heri wanablogu.

Faustine said...

Mzee! Hongera kwa ubunifu wako.
Nashukuru kwa salamu zako za Mwaka Mpya.
Nakupa pongezi za kutuunganisha mabloga kutoka Tanzania.

Nakutakia Heri ya Mwaka Mpya

Faustine
http://drfaustine.blogspot.com/

Unknown said...

Hi man!!
Nimeona ubunifu mzee, sio wa kawaida.
Umekamua mtu wangu, mashairi yametulia. vina ndio usiseme.
*****************************
Kwa niaba ya wanautambuzi wote na kwa niaba yangu menyewe, ningependa kuchukuwa nafasi hii kukushukuru kwa post yako maridhawa iliyojaa hekima na maudhui ya kiswahili mahiri.
Nakupongeza kwa ubunifu wako na nakutakia heri ya mwaka mpya, natarajia mwakani Blog hii itakuwa na mabadiliko makubwa, kwani mwaka mpya na mambo mapya, lakini usibadilishe falsafa yako hii tuliyoizoea.

Man, God Bless.

ERNEST B. MAKULILO said...

Mzee wa Changamoto,
Sijawahi on wala sikia eti mkono umepewa shukrani na mguu kwa kuutoa mwiba.Ila ni ujinga na upumbavu kwa mguu kutotoa shukrani kwa mkono, maana kuna miili mingine isiyokuwa na mikono, na mara ichomwapo na miiba hutaabika sana.

Mzee wa Changamoto,
Sitaki kuwa kama huo mguu ambao hauna shukrani hata kwa kutolewa mwiba. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati....kwanza kabisa kwa kuendeleza blog yako makini, na pili ni kwa UJEMBE muhimu sana wa kuga mwaka.Umetumia majina ya blogs za wadau karibia zote, na si tu kuzitaja majina bila ya kuwa na vina wala ujumbe...umehakikisha kila unapoweka jina la blog, ujumbe madhubuti tunaupata, mfano tumeona mchango wa kaka Issa Michuzi ktk uanzishaji wako wa blog.Nami alinisaidia ktk ushauri ufunguzi wa www.makulilo.blogspot.com

Nami nakutakia mmalizo wa 2008 mwema, na mkaribisho mwema wa 2009.Naamini tutazidi kupata mambo mengi na mazuri ktk blog yetu ya Changamoto.

MAKULILO Jr,

ERNEST B. MAKULILO said...

Mzee wa Changamoto,
Sijawahi on wala sikia eti mkono umepewa shukrani na mguu kwa kuutoa mwiba.Ila ni ujinga na upumbavu kwa mguu kutotoa shukrani kwa mkono, maana kuna miili mingine isiyokuwa na mikono, na mara ichomwapo na miiba hutaabika sana.

Mzee wa Changamoto,
Sitaki kuwa kama huo mguu ambao hauna shukrani hata kwa kutolewa mwiba. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati....kwanza kabisa kwa kuendeleza blog yako makini, na pili ni kwa UJEMBE muhimu sana wa kuga mwaka.Umetumia majina ya blogs za wadau karibia zote, na si tu kuzitaja majina bila ya kuwa na vina wala ujumbe...umehakikisha kila unapoweka jina la blog, ujumbe madhubuti tunaupata, mfano tumeona mchango wa kaka Issa Michuzi ktk uanzishaji wako wa blog.Nami alinisaidia ktk ushauri ufunguzi wa www.makulilo.blogspot.com

Nami nakutakia mmalizo wa 2008 mwema, na mkaribisho mwema wa 2009.Naamini tutazidi kupata mambo mengi na mazuri ktk blog yetu ya Changamoto.

MAKULILO Jr,

Mzee wa Changamoto said...

Sina zaidi ya shukrani. Najua vijiwe ni vingi lakini aminini kuwa kila mtazamo una elimu ya tofauti hata kama ni kuhusu mada ama picha moja. Bado utambuzi wa matatizo yetu unaendelea kutegemea namna tuonavyo hayo matatizo na kwa kuwa tu-wengi na twaona kwa mitazamo tofauti, tunaishia kuwa na mchanganyiko na mkanganyiko wa masuluhisho na hilo husaidia kupata lililo bora zaidi. Na hapa si juu ya nani aliye zaidi, bali kujua kuwa TUPO PAMOJA NA TUKIWA PAMOJA KWA UMOJA HAKITAHARIBIKA KITU.
Nawaheshimu nyote na uwepo wenu ukingali wahitajika.
Blessings

Fadhy Mtanga said...

Heri ya Mwaka Mpya kwa bloggers wote.
Na wasomaji wetu.
One love.

Koero Mkundi said...

Habari kaka Mubelwa,

Nakutakia heri ya mwaka mpya wa 2009.
Naomba tuendelee kushirikiana kama mwaka uliopita.

MARKUS MPANGALA said...

waungwana mnisaidie nitamweleza kuwa mwaka 2009 nimeuona. jamani mungu awe nasi upendo uwe nasi. PAMOJA DAIMA

Anonymous said...

Kazi nzuri Mzee wa Changamoto.Nakutakia kila la kheri wewe pamoja na bloggers wenzetu wengine wote katika mwaka huu mpya wa 2009.

Nimependa pia ubunifu wako katika post hii.Umetambaa na lugha maanake.

Egidio Ndabagoye said...

Heri ya mwaka 2009 kaka.

Anonymous said...

Mungu abariki kazi ya mikono yako!

Anonymous said...

Mungu abariki kazi ya mikono yako!