Tuesday, December 30, 2008

Una uhakika ni ndoto na si Ufunuo?

Naanza kwa kujiuliza tofauti ya ndoto na ufunuo. Maana najua wapo wafunuliwao wakiwa usingizini. Lakini ina maana kama yale waliyoofunuliwa hayatatokea machoni ama kusikika masikioni mwao wataendelea kuona huo kama ufunuo ama ndoto? Hapa ntahitaji msaada kidogo maana twatofautiana uelewa juu ya hili ama haya. Ninalomaanisha ni kuwa kama halijatokea kwako ama hujalisikia laweza kuendelea kuwa ndoto kwako, lakini kama ulishalisema kwa mtu na akaliona likitendeka huko aliko anaweza kuona ni ufunuo.
Sasa tukirejea kwenye CHANGAMOTO ZETU zitukabilizo kila siku, unadhani ni mangapi unayaota usiku ama ulalapo na unashindwa kuyatendea kazi? Sisemi kuwa uendeshwe na ndoto na majinamizi yakutumbayo usiku maana najua si yote ama zi ndoto zote senye nia ama mtazamo mzuri, lakini ni kweli kuwa hakuna haja ya kutilia maanani yale mema tuotayo? Je kuyasimulia?
Lucky Dube alisema "have you ever see the dream walking?, have you ever hear the dream talking? ....You are THE MASTER of your dream, if you pull the right string it'll be talking to you, don't hesitate, grab the chance before it's too late .... reach out and touch your dream" Akimaanisha (kwa tafsiri yangu) kuwa si vibaya kuangalia njia sahihi na muafaka ya kutimiza zile uonazo kama ndoto zako na kuna ukweli kuwa upo uwezekano ukafanikiwa. Lakini ni kama utachukua hatua hiyo ya kutekeleza hayo kwa wakati muafaka. Namkumbuka mmoja wa wahubiri niliowahi kuhudhuria ibada zake aliyesema "your mental picture will determine your actual future". Sasa hapa naunganisha na ile tafsiri kuwa tunaota yale tuwazayo. Ina maana tunawaza kwanza kisha tunaota. Kwa hiyo ina maana kuwa kwa namna moja ama nyingine hayo tuotayo (narudia tena si yote) yapo ndani mwetu. Au nimekosea? (Una haki ya kukosoa pia)
Ni wimbo huo huo ninapousikiliza nikakumbuka yale niliyowahi kuota nikiwa bwana mdogo na ambayo yamekuja kutimia baada ya juhudi na misaada ya wengi na kujiuliza kama nisingeweza kusaidiwa na kujishughulisha ningeweza kutimiza? Ina maana zilikuwa ndoto ama nilifunuliwa maisha yangu yajayo?
Tunapoanza mwaka ujao na tuwe makini katika kuupanga. Kumbuka yale upendayo ambayo umekuwa ukitamani, kuota na kujaribu kuyatekeleza lakini hukupata nafasi ya kujaribu. Yape muda na mipango sahihi ya kuyatenda na yawezekana yakabadili maisha yako.
Msikilize hapa chini akizungumzia namna ya kugusa ndoto zako.

KILA LA KHERI

3 comments:

Unknown said...

HABARI ZA SIKU KAKA,
TANGU JUZI SIJAPITA HAPA KIJIWENI KWA SABABU ZA PILIKA PILIKA ZA KUSAKA HABARI ZA KUWEKA KWENYE KIBARAZA CHANGU.
USIWE NA SHAKA MZEE TUKO PAMOJA.

Koero Mkundi said...

Habari za siku kaka.
haya mabo ya ufunuo na ndoto huwa yananitatiza sana.
Lakini kuna jambo nimejifunza kupitia makala yako.
God Bless as usual.

MARKUS MPANGALA said...

Eee bwana weee LUCK DUBE mungu ambanike pazuri mkuu ila amsamehe kuhusu lile jani. Mda tamu sana. nafikiri ni kwamba tunaweza kupata ufunuo na ndoto kwa wakti mmoja lakini funuo ni nini na ndoto nini, vilevile njia za kupata ufuuo zipoje na ndoto zipoje , lakini tunaweza kufanikiwa ikiwa ndoto zetu zina NIDHAMU, ikiwa ndoto zetu zimejaa ufunuo ambao kila daika imepewa kazi yake ya kufanya au kufikiri au hata kama kwa kupumzika.
Ndiyo ufunuo unaweza usiujue lakini ndoto utazijua kwa mengi ikiwa ni shemu ya fikra nyingi, ndiyo maana DUBE kasema ndoto hazitembei wala kuongea kwahiyo aongeaye ni mtu apanagye ni mtu, lakini anajua kwanini anandoto hzio na anaamini atapata ufunuo? maana nadhani ukiwa na ndoto basi ufunuo utafuata. sidhani kama ufunuo unaanza ndipo ndoto hufuata.
je tupo katika njia sahihi ya kujipa ndoto na ufunuo? pengine sijielezi vema. kwaheri kwa leo mkuu