Hali ya UCHUMI na maisha kwa sasa inasikitisha saana. Inaelekea ambako wasio nacho inakuwa ni zaidi ya mzigo na wenye mali bila imani wanatumia nafasi hii kujiweka katika mazingira mazuri ya taabu zijazo. Ni kweli kuwa kila kona ulimwenguni kuna maumivu kutokana na "mgogoro huu wa kiuchumi" unaoendelea. Haijalishi ni makosa ya nani wala ni nani wa kulaumiwa, sasa ni wakati wa kuweka imani mbele na kutenda yale tutakiwayo kutenda. Kwa wale wenye imani na tuendelee kumuomba Mngu atuwezeshe katika kile alichotupangia maana "ni yeye aonaye na kujua yale tunayopitia sasa ili kutengeneza maisha yetu n a ni yeye aonaye na kujua ni umbali gani umebaki kabla hatujafikia mafanikio yetu." Tumuombe atusaidie tusikate tamaa na atuwezeshe kufika tuendako salama.
Ni siku ambayo kwa ufupi wa maneno hayo, nawaacha naye Jephter Washington McClymont ama Luciano ama Jah Messenger akisema God you see and know. Ukisikiliza maneno kwa makini utatambua kuwa ni wimbo muafaka kwa hali ya maisha yetu ya sasa.
Enjoy and stay BLESSED
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Changamoto yetu sote, mimi wewe yeye yule,
Tutafutapo mkate, tuyajue mambo yale,
Mambo sasa ni magumu.
Dunia yatingishika, vipi kwa taifa letu?
Tujipange kwa hakika, tujifunze kwa wenzetu,
Mambo sasa ni magumu.
Uchumi unapoyumba, tumkimbilie nani?
Tushazowea kuomba, tutakufa masikini?
Mambo sasa ni magumu.
Ni magumu kweli kweli, werevu walishaona,
Tufikiri mara mbili, ni vipi twaweza pona,
Mambo sasa ni magumu.
Asante mzee wa vina Kaka Fadhy. Naamini ni kwa wote na twaweza kuungana kuweka maombi na mitazamo iliyo chanya kuunganisha juhudi zetu.
Blessings
KAKA NIMEIONA CHANGAMOTO.
KAAAAZI KWELI KWELI!!!!!!!!!
Post a Comment