Thursday, December 25, 2008

KRISMAS NJEMA


Napenda kuwatakia ndugu, jamaa na marafiki HERI YA KRISMAS. Natambua kuwa kila sikukuu ya ki-Imani huambatana na mafundisho yatufaayo maishani. Ni kwa hili naomba kushirikiana katika kuyatekeleza mafundisho hayo sio tu kwa siku ya leo, bali maishani. Hii itatufanya tuishi kwa AMANI, HESHIMA UPENDO NA UNYENYEKEVU mbele ya wenzetu na MUUMBA wetu

HERI YA KRISMAS

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kRISMAS NJEMA NAWE PIA. MUNGU AKUBARIKI

Koero Mkundi said...

Mzee wa Changamoto, mimi ni mgeni, nimepita hapa kujitambulisha naipenda sana kazi yako. karibu kwenye kijiwe changu, unisaidie kukiboresha.

ni mimi Koero Mkundi

Mzee wa Changamoto said...

Asante sana Da Yasinta kwa Baraka zako za kila siku. Pia Mdau Koero nakukaribisha sana. Si hapa tu, bali kwenye ulimwengu mzima wa ku-blog. Ni kweli kuwa kutembelea vijiwe hutufanya kupata mengi ya kuweza kuboresha "majamvi" yetu. Karibu saana na kuna sehemu nyingi sana za kupitia na waweza kuziona kwa kubofyabofya "blogscroll" hapo "sebuleni".
Krismas njema

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

Asante kaka! kazi njema, Mungu abariki kazi ya mikono yako. Amen