Friday, December 26, 2008

Them, I & Them. LUCIANO: Why

Jephter Washington McClymont "Luciano"
"Why can't the children of the world unite, and why can't the mankind live right and when will the leaders of this world realize, that the ship is about to capsize, and when will there be any peace on earth, when human kind know what life is really worth"
Ndio maneno aanzayo nayo Luciano, mmoja wa wasanii "wema" sana wa muziki wa Reggae ulimwenguni katika wimbo wake alioupa jina la WHY. Wimbo ambao amejiuliza mengi kuhusu ulimwengu kuanzia viongozi mpaka wananchi wa kawaida. Luciano anauliza mengi katika wimbo huu akiendelea kusema kwanini twahitaji kupigana kutetea kile ambacho MUNGU ametupa kama haki yetu akisema "..why do we really have to fuss and fight, to defend our GOD-given right" na pia anaendelea kuuliza "...and why should we live our lives like this, when we know,for sure that Jah is here..."
Maswali ni mengi lakini twatambua kuwa wa kujibu haya ni sisi wananchi na wale wafanyao maamuzi ambayo wakati mwingine yanaumiza wasio na uwezo na ama nafasi ya kufanya maamuzi hayo.
Bofya Player hapo chini kumsikiliza Luciano akiuliza WHY toka katika albamu yake ya Great Controversy

Ijumaa njema
Waweza kujua mengi kuhusu Luciano kwa kutembelea tovuti yake ya www.lucianoreggae.com
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**

3 comments:

Unknown said...

Why, Why, Why?. hata mimi naweza kuuliza why.
kuna mwana hip hop mmoja wa Kimarekani anaitwa JADAKISS, nae ana wimbo wake mmoja kauita WHY? katika wimbo huo kamchambua vibaya bwana Joji Kichaka.
naomba utuwekee huo wimbo hapa kibarazani kwako tuusikilize kama unaweza kuupata.

Koero Mkundi said...

Kaka Mtwiba, unanifanya sasa nianze kusikiliza hii miziki ya kimapinduzi.

Basi nikuchekeshe, Zamani nilidhani watu wanaopenda Hii miziki ya Reggae na kufuga Rasta, wanavuta Bangi. ambayo kimazoea tumefundishwa kwamba ni mbaya.

nilikuwa na Rafiki wa kiume, Rafiki tu, maana msije mkatafsiri vibaya, kwani mwenzenu mimi bado nasoma.
Basi yule kijana alikuwa anafuga Rasta na alikuwa mtanashati kweli.

Alikuwa anawachukia vijana wenzake wanovuta bangi na hata wale wanaofuga Rasta lakini wachafu..
Yeye ndie aliyenifanya niwaone watu wanaopenda Miziki ya Reggae na kufuga Rasta, katika jicho tofauti na jamii inavyowafikiria.
naamini kupitia katika blog hii nitajifunza falsafa hii kwa undani zaidi.

Mzee wa Changamoto said...

Ndio Dada Koero, mtazamo wa wengi juu ya vingi hutatanisha. Kama jina lisemavyo kuwa "namna uonavyo tatizo laweza kuwa ndio tatizo" nawe umedhihirisha kuwa ulivyokuwa ukiwafikiria hawa wenye Dreads ni tofauti na wengine walivyo. Siwezi kusema kuwa si kweli kuwa wapo wavutao bangi, lakini ntasema kuwa Rasta si sababu ya kufanya hivyo. Pia kuwa na dreadlocks hakumpi mtu imani ya u-rasta na urasta haumlazimishi mtu kuwa na dreadlocks. Waweza pia kutokuwa na vyote nikimaanisha kuwa waweza kutokuwa Rasta na usiwe na Dreadlocks na bado ukapenda Reggae. Kwangu mimi ntabaki na siri yangu, lakini najua kuwa naipenda Reggae kwa kuwa inanigusa katika kujitambua na kutatua matatizo yetu na hasa kwa kuwa wengi wa wasanii wa Reggae (na hapa nazungumzia roots reggae) hujihesabu kama wa-afrika wenye nafasi ya kutetea wanyonge. Na ndilo utakalokuwa ukilipata hapa siku za Ijumaa kwa kusikiliza yale yahusianayo na jamii yetu kutoka kwa wasanii hawa wa Reggae.
Asante kwa maoni na historia ya mabadiliko yako.
Blessings.
Kwako Kaka Kaluse nashukuru kwa kumsikiliza Luciano na kusikiliza swali la Why. Nausaka wa Jadakiss nione alisemaje lakini nadhani unakumbuka ile video iliyopo kwenye wimbo wa Pink niliouweka hapa Des 2 ambao alikuwa akimueleza Rais wake. Unaukumbuka? Uko kwenye label ya Politics Fix ambapo napo alimweleza Rais wake ayaonayo.
Ntasaka wimbo na nikiunyaka ntaubandika.
Blessings Man