Pengine yaweza kuonekana kama ndoto, na pengine yaweza kuonekana kama ni kitu kisichowezekana, lakini kwa hakika ni jambo linalowezekana. NAZUNGUMZIA KUTOKOMEZA UKIMWI NCHINI NA DUNIANI.
Japo ni kitu kiwezekanacho, lakini chahitaji jitihada za ziada. Twahidaji malengo na pia utekelezaji wa nia. Twahitaji kubadilika na kuacha kufanya ugonjwa huu kama mradi. Kisha kwa pamoja kuungana na walioathirika katika harakati zao za kuwa wazi. Wakiacha kunyanyapaliwa, wakapendwa, kuheshimika na kukubalika ndani ya jamii, watakuwa wazi zaidi kueleza namna tofauti walizopitia kufikia hali hiyo na kwa kufanya hivyo tutaepusha maambukizi mapya na kurefusha maisha ya wale wenye virusi hivyo. Japo idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huu vimeonekana kupungua kwa mwaka 2007 kwa mujibu wa TAKWIMU ZA W.H.O, bado tuna kazi ya ziada kuhakikisha tunawezesha namba ama takwimu hizi kufikia sifuri, yaani kuutokomeza ugonjwa huu.
Na hii ni CHANGAMOTO YETU sote.
Kuutokomeza ugonjwa huu wa UKIMWI...... NDIO TWAWEZA
Tumwangalie dada huyu alivyoelezea namna alivyopokea matokeo ya vipimo vyake. Amekuwa muwazi juu ya hali yake, amekuwa mwelimishaji na mwanaharakati mwema kuhusu ugonjwa huu
Video yake kamilifu kuhusu biashara mbaya ya kuuza mwili pale UWANJA WA FISI waweza kuipata kwa kutembelea http://www.hyenasquare.org/
Basi tusikie wasanii nyota wa Uganda wanavyoungana kwenye mapambano haya muhimu juu ya gonjwa hili hatari.
Ama twende CONGO ambako nao pia waliungana na kutoa kibao hiki kuhusu ugonjwa huu wa UKIMWI

3 comments:
UKIMWI jamani mbona utamu upo mlangoni na ubaya upo chumbani? kazi kweu waungwana.
nimemaliza mkuu
Wenzenu wanaungana ktk siku kama hiyo ili kuwatia moyo waadhirika,jamaa wanauwezo mkubwa kwa voco si mchezo,Wabongo lini mtafanya kitu km hiki wanamziki wote?kazi kusemana tu kuimba hamuwezi kazi kweli kweli.
Thx Anon. Lakini nadhani hatustahili kuungana just kuwatia moyo waathirika. Bila kuungana kuzuia maambukizi mapya basi tutatiana moyo mpaka tukose wa kumtia moyo mwenzake. Nadhani tuungane kupambana nao huku tukitiana mioyo.
Blessings
Post a Comment