Sunday, December 7, 2008

Ras Nas ndani ya Dokkhuset, Trondheim, Norway

Ras Nas
Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya muziki wa Dansi na Reggae, Nasibu a.k.a Ras Nas, yuko tayari kufanya vitu vyake katika jiji la Trondheim, Norway, usiku wa Ijumaa tarehe 12 Desemba. Kwa mujibu wa Ashley ambaye ni Meneja Uhusiano wa Kongoi Productions, katika onesho hilo linalotazamiwa kuwa ONESHO LA MWAKA, Ras Nas ametayarisha kikosi kikali chenye wanamuziki toka Congo Brazzaville, Ivory Coast na Sweden. Kwa tahadhari, asiye na mwana itabidi aelekee jiwe! Shoo itaanza saa nne na nusu usiku. Kabla ya hapo DJ Roar Lund atakuwepo uwanjani kufyeka msitu.

Kwa maelezo zaidi Bofya Hapa (kiinglish)
NYOTE MWAKARIBISHWA

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Asante sana kwa taarifa. Norway ni nchi jirani na sweden kwa hiyo nitajitahidi kwenda ni saa moja tu.

Anonymous said...

Kaka Mubelwa, blog yako nzuri sana especially nimependa sana hiyo PARADOX OF OUR TIME. Asante kwa kutembelea blog yangu. Endeleza hii kazi nzuri ya kutuelimisha.

Mzee wa Changamoto said...

Karibu na ASANTE kwa kutembelea hapa Da Sophie. Da Yasinta wewe mwenyeji na nashukuru kwa kurejea tena kunijulia hali. Mbarikiwe