Saturday, January 31, 2009

Hivi kuna bahati? Na kama ipo si ni lazima iandaliwe?

Ukijiuliza ama kuuliza swali la NINI MAANA YA BAHATI utaweza kupata majibu mengi sana. Nilipowauliza "waungwana" nifanyapo kazi wamekuwa na majibu tofauti, lakini mengi ni yale yenye mtazamo kuwa bahati ni kile kikutokeacho na kwa manufaa yako bila kukugharamisha wakati kikitokea. Nikaanza kujiuliza kwanini watu wanadhania hivyo (kwa mtazamo wangu) nikagundua kuwa ni kwa kuwa hawarejeshi mawazo nyuma kuona kunakomfikisha mtu abahatikaye kubahatika.
Binafsi siamini kama kuna bahati isiyoandaliwa. Ni lazima mtu awe kwenye mahala, nafasi ama mazingira fulani kuweza kubahatika. Kuna elimu, harakati ama chochote mtu afanyacho kujitengenezea mazingira ya kubahatika ambavyo wengi wetu hatuvioni ama hujilazimisha kusahau hasa pale tunapotaka kuamini kuwa mwenzetu kabahatika. Mfano ni pale mtu anaposhinda bahati nasibu. Lazima ujue kuwa hata kama ana bahati kiasi gani, hawezi kushinda bila kuweka juhudi za kununua kadi ama kama amepewa kuwa na ujasiri wa kuikubali. Wanaoteuliwa kuchukua nafasi za wanaojiuzulu ama kufa ni lazima walikuwa na elimu fulani ama wamefikia viwango vya kuwawezesha kutwaa nafasi hizo.
Ukiangalia kwa makini juu ya kile unachoona kilikutokea kama bahati, utagundua kuwa ulikuwa ni mtu sahihi, mahala sahihi kwa wakati sahihi na ndio maana yamekukuta ama umepata hiyo uiitayo bahati.
Fikra ya kuwa twaweza kubahatika wakati mwingine ndio inayotufanya tupande mbegu za usembe na uvivu kwa wengine kuwa wapo wenye bahati za kuwa kina fulani na wengine hawajaumbwa na bahati hizo, hivyo kuwafanya watusikilizao na kutuamini kuacha kuweka juhudi kwenye yale ambayo yangewajengea mazingira mazuri ya "kubahatika". Ni huu mtazamo wa bahati unaosababisha watu kuendelea kutegemea "nafasi za upendeleo" kuweza kuendelea.
MTAZAMO WANGU ni kwamba kila mtu afanye maandalizi ya kile apendacho kufanya maishani kielimu na kiutambuzi kisha kuna wakati utakapokuwa mahala ambapo utakutana na mazingira yatakayokuaminisha kuwa umebahatika (kama unaamini katika bahati)
Katika albamu yake ya Trinity, Lucky Dube aliwahi kuimba wimbo AFFIRMATIVE ACTION ambako amemuonya kijana Georgie kuacha kuangalia maisha kwa mtazamo wa bahati na kutegemea nafasi za upendeleo. Anamwambia "Education is still the key. Even though we have Affirmative action"
Naweka wimbo na maneno yake nawe sikiliza na kusoma. Kisha ujiulize kama kweli kuna bahati isiyoandaliwa

Education is still the key
Even though we have Affirmative action.

From where I stand I can see the world getting smaller and smaller
And there'll be no place for people like you Georgie who still live in the past
When you couldn't do things for yourself, you blamed it on apartheid,
You blamed it on the government and everybody
Now is the time to prove yourself
If you think affirmative action
Is the way out... no way... no way.

Constitution can be changed from time to time,
But that does not mean that you don't need no education
We are tired of people who think that affirmative action is the way out
And, is another way of putting puppets where they don't belong

I'm so sorry Georgie but the only way to get our economy strong,

is to have an educated nation.
And if you think affirmative action
Is the way out... no way... no way.

Chorus
Education is still the key
Even though we have Affirmative action.

Chorus till fade.

6 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

bahati mbaya, bahati nzuri. kama hakuna bahti, je kuna mkosi? sijui lakini tafsiri yako ndo ina mata zaidi ya bahati. kuna watu wanaoitwa bahati na hivyo labda kuna bahati maana ukimwita ataitika na kukufuata. proof

Anonymous said...

Mzee wa Changamoto hongera zako nimeona comment yako hapa http://koeromkundi.blogspot.com/2008/12/hivi-kwa-nin-i-tangu-mwaka-1947-hadi.html

Nimeipenda briefly inasema "no research no right to say" . Endeleza kazi yako nzuri unayoifanya katika uwanja huu wa blog. Unatoa mwongozo mzuri.

Koero Mkundi said...

nasikitika kwamba wanasiasa hapa wanaichezea elimu........

Kila siku najiuliza na sitaacha kujiuliza, hivi wanasiasa wetu wanatumia aina gani ya ubongo katika kufikiri?
wanajisikia vipi kuona nchi ikiwa bado katika lindi la umasikini wakati muumba aliibariki nchi hii kwa rasilimali chungu mzima.....

Nadhani itafikia wakati wajukuu zetu watakwenda kufukua makaburi yao na kutoa mafuvu yao ili kuyapima kama yalikuwa ni ya watu wa aina gani?
Na huenda wakayatemea hata mate...

MARKUS MPANGALA said...

Sijui ni bahati au kama enzi zile tusemavyo zali! watambuzi tusaidieni.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ni kweli hakuna bahati wala zali kila kitu huwa tunajipangia na kujiamulia. na ndivyo hivyo kusivyokuwep o na jambo baya au zuri maishani. huwa kuna matukio tu na kifuatacho nitafsiri.

hakuna bahati, hakuna mkosi, hakuna jambo zuri wala baya. koero analalmikia wanasiasa badala ya kuchukua hatua. mashujaa wote tunaowasoma, walijitoa kukemea upuuzi. kwa hiyo koero kama unaona noma kwen siasa zetu, hebu simama kidete ukemee, na mambo yatanyooka na hivyo kuwa bahati kwako kwamba hutafutika kwenye historia. mikakati yako ndiyo itakayokuwa imekuletea bahati wakati kulialia kwako hakutabadili lolote na kubaki kumtafuta mchawi mwishowe kujiona mwenye mkosi mkuuuuuubwa

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Umesema kweli Mzee wa Changamoto - hakuna bahati isiyoandaliwa - pengine kwa watu wa dini wanaopata miujiza, au watu wachache sana wanaoshinda bahati nasibu au kuokota rundo la pesa. Vinginevyo ni lazima bahati uifanyie kazi. Mtazame raisi Obama kwa mfano. Alianza kujiandaa tangu akiwa Oriental College kule Los Angeles. Huko ndiko alitoa hotuba yake ya mwanzo na anasema alifurahia sana kuisikia sauti yake na mwangwi iliousababisha na kuona wanafunzi wenzake wakimpigia makofi. Kutoka wakati ule kila alichokifanya alijua kwamba siku moja kingekuja kumsaidia katika ndoto yake ya kuwa raisi. Ndiyo maana aliweza kutotenda mambo mabaya ambayo baadaye yangekuwa kashfa na kuzima ndoto zake. Ndiyo alijaribu madawa ya kulevya na bangi (na amesema hivyo katika kitabu chake) lakini hii inamwonyesha kwamba naye ni mtu wa kawaida tu na siyo malaika. Ukisoma vitabu vya watu wengi mashuhuri na waliofanikiwa utagundua kwamba wengi wao walikuwa wamejiandaa vizuri, walikuwa na ari na walikuwa katika wakati mwafaka na ndiyo BAHATI ikawajia