Thursday, January 15, 2009

Maisha ni taswira, lakini ........

Mchungaji wangu aliwahi kuniambia kuwa "your mental picture will determine your actual future"
Pengine hata ulipoangalia kichwa cha leo ukawa na picha ama taswira ya nini chaweza kuwa chazungumziwa ndani mwake. Lakini pia suala la kutambua ni kuwa kwanini tunakuwa na taswira na je nini chanzo cha taswira na kama zote zafaa maishani mwetu.
Mwandishi Dave Ellis ameandika kuwa taswira ndizo ziongozazo fikra zetu, maongezi yetu, matendo yetu na kwa ujumla kuendesha maisha yetu. Na tatizo (kwa mujibu wa mwanasaikolojia William Glasser) ni kuwa akili zetu ni kama albamu ambayo hujaza taswira za namna tulivyofanikiwa kutimiza haja zetu zilizopita na pale tunaposhindwa kutimiza basi husaka zile taswira za zamani na kutaka kulazimisha ulimwengu wa nje kukubaliana na taswira za ndani.
Tatizo la taswira ama picha zilizopo akilimwi mwetu ni kwamba zatuzuia kuuona ukweli kuhusu sisi na maisha halisi tuishiyo. Ni taswira za mahala fulani zitufanyazo tudhani pako hivi ama vile ilhali yawezekana kusiwe na ukweli halisi wa hilo na ikitokea kukawa tofauti basi twasononeka na kuvunjika moyo. Ama mitihani na ama mtu unayetegemea kukutana naye ambaye kwa kuzungumza naye kwenye simu ama ku-chat wajenga taswira ambayo yaweza isiwe na ukweli wa alivyo, a inapotokea ikawa vinginevyo basi twakasirika na ama kusononeka.
Tatizo kubwa ni kwamba, kwa kuwa hatuna uwezo wa kuzidhibiti taswira akilini mwetu tunakuwa na uwezo mdogo wa kudhibiti sehemu ya maisha yetu (kumbuka zatusaidia kuhisi, kuongea, kutenda na kufikiri).
Moja kati ya njia za kukabiliana na taswira na picha hizi akilini mwetu ni kwa kuzitambua. Tambau picha zinavyoathiri mawazo, hisia na matendo yako. Kisha mara utambuapo taswira hizi zikiwa ndani ama zikiingia akilini mwako, basi zitambue kisha ziruhusu kwenda. HUWEZI KUPINGANA NA TASWIRA maana hata uziachiapo hurejea tena na tena. La muhimu ni kuruhusu ziingie kisha uzitambue kuwa sizo upendazo na baada ya hapo uziache ziende
Dave Ellis ameandika kuwa " you can let pictures go without giving up yourself" na kisha akaongeza kwa kutuhakikishia kuwa "we can take charge of the images that floats through our minds"
MAISHA NI TASWARIA KWA KUWA ZINAONGOZA UKWELI NA HISIA ZA MAISHA YETU, LAKINI TWAHITAJI KUZITAMBUA, KUZICHUJA NA KUZITUMIA KWA UANGALIFU KWANI NI MUSTAKABALI WETU.

5 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

taswila. the power of postive thinking, the power of now, sijui nini

Mzee wa Changamoto said...

Kuna nguvu saana katika kufikiria mtazamo chanya na huo hutuwezesha kuwa chanya pia

Simon Kitururu said...

Lakini taswira za maisha zinaweza kuwa zimetandiwa ukungu!:-( Unaweza ukajikuta uko njia panda, kwa shetani uasherati ukunogeao, bia zipo na ...., kwa Mungu kuna kupiga magoti na kunyenyekea ukubalike mbinguni kwa ajili ya kuishi milele kitakatifu!

Taswira ya maisha inaweza kukufanya kushindwa kuchagua kombi ya kusomea ukiwa Form Four.

Mzee wa Changamoto said...

Asante Kaka Simon na karibu tena. Tofauti ya taswira huleta na kutupeleka sehemu na katika hali mbalimbali na ndio maana sentensi ya mwisho nikasema "MAISHA NI TASWARIA KWA KUWA ZINAONGOZA UKWELI NA HISIA ZA MAISHA YETU, LAKINI TWAHITAJI KUZITAMBUA, KUZICHUJA NA KUZITUMIA KWA UANGALIFU KWANI NI MUSTAKABALI WETU."
Blessings

Simon Kitururu said...

Nilikuelewa Mzee!Nilikuwa namwagatu sentensi zaidi ndani ya hoja.