Monday, January 26, 2009

Them, I & Them...INNOCENT NGANYAGWA...Sumu ya Udhalimu

Katika moja ya matoleo ya jana kuna makala iliyoandikwa na Kaka Ernest Makulilo juu ya TANZANIA NA DHAMBI YA UBAGUZI WA RANGI. Ameandika mengi na amechambua kuhusu mtazamo na kisichoeleweka juu ya kwanini na ni vipi mtu anaweza kufanya ukatili wa namna hiyo kwa mwenzake kwa kisa ama sababu ya rangi.
Tulishaonywa na Baba wa Taifa juu ya dhambi ya ubaguzi. Msikilize Inno Nganyagwa alivyoimba miaka 6 iliyopita juu ya SUMU YA UDHALIMU ambapo humo kuna kipande cha hotuba halisi ya Hayati Baba wa Taifa Mwal Nyerere alipozungumzia kuhusu DHAMBI YA UBAGUZI NA UGUMU WA KUITOKOMEZA UKISHAITENDA

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

MARKUS MPANGALA said...

Hii ni changamoto kwetu kama kizazi ambacho kinakabiliwa na ubinafsi kupindukia. Tunatakiwa kuona ukweli kwamba tuendako siko kule tunakotoka kila leo. Ni jukumu letu wananchi wewe na mimi, na maoni yetu ni jinsi gani tutaweza kukomesha haya mambo

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mambo ya albino sio ubaguzi bali tatizo ni dini zenu hizi za miujiza kwa kwenda mbele.
ila mimi sielewi vizuri dhana ya ubaguzi wa rangi ninini, sijui kama hupo ila kuna kujilinganisha. kuna wanaojiona bora kuliko wengine na kufanya vituko sasa na wewe unatamani kuwa kituko kama wao eti ni haki! mi cjui ila wenye haki waliishakufa.

maalbino nao wanapendekeza wanaowauwa wauwawe, nani kasema dawa ya moto ni moto na sio maji, mvua wala upepo?