Friday, January 16, 2009

Them, I & Them. LUCKY DUBE.........Soldier

Athari za vita ni zaidi ya tuzionazo kwenye vyombo vya habari. Kuna athari za kimawazo ambazo huwakuta askari wa pande zote (wanaosema wameshinda na walioshindwa) ambazo hukaa nazo kwa muda mrefu wa maisha yao kulingana na yale waliyoona ama kutenda. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, hadi kufikia mwisho wa August mwaka jana kulikuwa na uwezekano wa idadi ya askari wanaojiua baada ya utumishi wao vitani kuvunja rekodi hapa Marekani (Bofya hapa kusoma taarifa hiyo).
Lakini haya alishayaona na kuyaimba Lucky Dube katika wimbo wake Soldier ambapo alimnukuu askari akisema "I can't change the past but I can change the future. If I pull this trigger right now, right here, everything will be over. Not a day goes by I don't see them in my dreams, not a day goes by I don't hear them screaming in my ears begging for mercy, pleading innocent. Since my heart is made up to be as cold as the barrel of this gun I hold I would pull the trigger anyway" Na katika sehemu ya kiitikio ambayo ni kama Askari akielezea kilichosababisha yote hayo (ambayo ni kama vile hakutaka kuyatenda, anasema) "I was a soldier, following instructions from a man we have known as the general".
Ni majuto ambayo yamemfanya afikirie kujiua licha ya kupata medali na tuzo nyingi kwa yale ambayo amefanya ambayo licha ya kufichwa na serikali bado yanamsumbua kwa ndoto na majinamizi ya yale aliyowatendea wasio na hatia ambapo anasema "so many medals, so many praises. Nothing can take away the guilt that I feel inside me. Government covered up every crime we committed against human kind. Not a day goes by, I don't see them in my dreams, not a day goes by, I don't hear them crying in my ears"
Pengine ni wakati wa kuangalia yale ambayo kila mtu anayafanyia maamuzi maana hata kwa wale wanaosherehekea "mafanikio na ushindi" katika vita, kuna athari nyingi kwa askari na familia zao maana wapo wanaoua wenza na watoto wao kabla hawajajiua wenyewe.
Msikilize Lucky katika wimbo huo uliokuwemo kwenye albamu ya The Other Side. Ameanza kwa "Chant" ya "matching band" ambayo pia ameitumia kwenye kiitikio anayosema "stand for the truth you stand alone, government will cover up" kisha inafuata midundo maridhawa ya Reggae iendanayo na maudhui.

Stand for the truth you stand alone
government will cover up
i saw a man sitting in a room
holding a gun to his head
he said man oh man
what am I gonna do
I can't change the past but I can change the future
If I pull this trigger right now, right here
everything will be over
not a day goes by I don't see them in my dreams
not a day goes by I don't hear them screaming in my ears
begging for mercy, pleading innocent
since my heart is made up to be as cold
as the barrel of this gun I hold
I would pull the trigger anyway

Chorus
I was a soldier, following instructions from a man
we have known as the general

Stand for the truth you stand alone
Government will cover up

so many medals, so many praises
nothing can take away the guilt
that I feel inside me
Government covered up every crime we committed
against human kind
not a day goes by, I don't see them in my dreams
not a day goes by, I don't hear them crying in my ears

Chorus
Stand for the truth you stand alone
Government will cover up.

IJUMAA NJEMA

5 comments:

Koero Mkundi said...

Ngoja ninukuu hiki kipande.

"so many medals, so many praises. Nothing can take away the guilt that I feel inside me. Government covered up every crime we committed against human kind. Not a day goes by, I don't see them in my dreams, not a day goes by, I don't hear them crying in my ears"

Hiki kipande kimenigusa sana,
Kwa wale waliosoma Baioloji watakubaliana na mimi kwamba katika ubongo kuna eneo linalohusika na kuweka kumbukumbu

Huwa najiuliza inakuwaje kwa yule ambaye ameshuhudia au ameshiriki katika mauaji vitani?

Hebu tutafakari future ya wale watoto wa Iraq, Palestina, Liberia,Siera Leon, Rwanda, Burundi, Congo DRC, Ugandana kwingineko, Je mustakabali wao na matarajio yao katika maisha utakuwaje.

Nakumbuka Mtambuzi katika mojawapo ya makala zake aliwahi kuandika, "Mtu akiuwa vitani ni shujaa, lakini mtu huyo huyo akiua uraiani ni muuaji anayestahili kunyongwa"

Mimi naoana muuaji ni muuaji tu awe ameuwa vitani au uraiani.

Lakini jamii imetengeneza misamiati ili kuhalalisha mauaji.

Hebu tujiulize, Hivi mtu kupewa medali kwa kuuwa vitani ni ushujaa au ni laana?

kama mtu unavalishwa medali eti kwa sababu ya kuuwa vitani, hiyo haithibitishi kwamba mikono yako imetapakaa damu ya watu wasio na hatia?

Lakini ukitafakari sana, utagundua kwamba WANASIASA ndio chanzo cha hii migogoro yote ya kivita tunayoishuhudia.

Ndio maana najiuliza, hivi ni lini dunia hii itakuwa ni mahali pa amani, watu wakiishi na kufaidi matunda ya kazi zao.

Christian Bwaya said...

Huwa nashangaa. Kwa nini kila wakati dunia ikibahatika kupata mtu mahususi kwa ajili ya ukombozi wa watu wake, ghafla anatoweka?

Koero Mkundi said...

Kaka Bwaya, wema huwa hawadumu.
Nitaandaa makala kuzungumzia hilo wiki ijayo, bado nakusanya ushahidi.
Lakini wakati nikiendelea na utafiti wangu hebu tutafakari wote kuhusu watu hawa,

Sheghu Shaghari, Patrice Lumumba, Nkuruma, Martin Luther King Jr., Edward Moringe Sokoine, Malik Shabazz, aka Malcom X, J F Kennedy, Chacha Wangwe, Bob Marley, Peter Tosh, Lucky Dube, Bantu Holomisa, na wengine wengi ambao sikuwataja lakini wanao wasifu unaofanana na hao niliowataja.

Je,kuna yeyote anayekumbuka waliyoyafanya wakati wa uhai wao?

Mzee wa Changamoto said...

Nasubiri makala Dada. Asante kwa kutukumbusha. Kaka Bwaya hiyo ni changamoto na twapaswa kuitafakari. Ni kama umetupa hints za kuanza kufikiri nini tutajaza kwenye makala ya Da Koreo

Evarist Chahali said...

Nimepita hapa chapchap kutoa salam.R.I.P Lucky Dube!