Friday, February 6, 2009

Them, I & Them... NASIO: Dangerous

Rais J.M Kikwete (Tan) akikabidhi madaraka ya AU kwa Rais Muammar Ghadafi (Lib)
Moja ya habari ambayo imetawala Afrika wiki hii ni kumalizika kwa mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika ambao walikutana huko Addis Ababa Ethiopia ambapo licha ya kutangazwa kwa kiongozi aliyeonekana kuuanza uongozi kwa staili na matakwa yake, lakini pia tumeshuhudia hotuba nyiingi toka kwa viongozi ambao wamezungumza mengi kuhusu wenzao na kupuuza ukweli wa matatizo yaliyojirundika nchini mwao.
Sijasikia lolote kutoka kwa rais yeyote kuhusu nchi yake. Sijasikia lolote la maana zaidi ya kunyoosha mapito ya matendo ya viongozi hawa na kunyoosheana vidole. Hivi ni kweli kuwa kuna nchi yoyote kati ya wanachama 53 wa AU ambayo haina matatizo ya kutatua kiasi cha kuanza kuangalia ya wenzao na hata "kuota" nchi moja ya Afrika?

Na ndipo ninapoungana na Nasio leo katika Them, I and Them katika wimbo wake DANGEROUS ulio kwenye albamu yake ya Living In The Positive aliyeanza kwa kusema "Speak the truth and speak it over. Love God and leave, is my only destination. Yeah, i heard your speeches, man and your empty promises (promise is a confort to a fool), but now that i know, your words are dangerous" na anaendelea kuimba mengi juu ya yale wanasiasa watumiayo kudanganya kisha anataja yale wapendayo kujitetea ilhali wenye uhitaji wakiwa wahanga wa maamuzi yao akisema "i heard them saying, there are only bribings, Lord the babes and the sucklings, making promises they can't keep and them never will. I see so many innocent begging for the guilty, but the blind is the victim in the land of evil sighted. Where there's no vision, man the people suffer, see them cornered by their judgements, and they're consumed by their hatred."
Unaweza kusoma na kujua mengi kuhusu Nasio kwa kubofya hapa. Lakini sasa msikilize Nasio hapa chini na ujumbe kwa viongozi wa siasa ambao wamepoteza imani kwa wengi katika kibao hiki DANGEROUS


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

1 comment:

Subi Nukta said...

Mara nyingi nyimbo ni jibu la maswali mengi sana kwa sababu huwa inasaidia msikilizaji kutambua kuwa wapo na wengine wanaoliona tatizo na kwa wakati huo kufarijiana na kusambaza ujumbe.
Siasa si hasa bali visa na mikasa tu!