Friday, March 6, 2009

Them, I & Them. NASIO........WHEN

Picha hii ya mwaka 2008 yaonesha Kambi ya Kalma huko Sudan ambako watoa msaada wameondoka baada ya kutolewa hati ya kushitakiwa kwa Rais Omar Bashir ambako kunaweza kuanzisha vurugu.
Hizi taswira za za kusikitisha za mwaka 2007 zinaonesha yaliyokuwa yakitendeka huko Darfur Sudan ambako watu waliuawa kwa kuwa walikuwa wakionekana ni wa ngozi fulani. Yaani mwonekano wao ulikuwa tatizo na ndio kilikuwa chanzo cha mauaji makubwa na ya kutisha. Nakumbuka alivyoimba Bob Marley aliposema "until the colour of man skin, is of no more significance than the colour of his eye, there will be war". Pengine wapo wanaoweza kushangaa kuhusiana na vita hivi vya wenzetu huko Darfur kwa mtazamo wa rangi, lakini wangeanza kujiuliza vita ni nini? Na kisha tujiulize vyamuathiri nani na kwanini?
Wiki hii Mahakama ya kimataifa imetoa mwito wa kufunguliwa mashtaka kwa rais wa Sudan Omar Al Bashir kwa yale yaliyotokea huko Darfur (kwa kuwa amehusishwa na hilo) na japo mchakato mzima unaendelea, bado kuna tetesi za mauaji na vita ambavyo vimesababisha watoaji misaada wameondoka sehemu hizo wakihofia kuanza upya kwa vurugu zinazoweza kusababishwa na tangazo la mashtaka kwa Rais (Bofya hapa usome). Ni vita hivi vinavyoendelea kuwakuza watoto kwenye mazingira ya ajabu na ambayo yataathiri ubongo wao maisha yao yote na watu wazima wanaendelea kuishi bila matumaini.
Ni lini watoto hawa watatoka nje wakaenda kucheza bila kuhofia mabomu na risasi? Ni lini watu wa Sudan watarejea makwao na kuishi wakiifurahia amani?
Namleta kwenu Nasio wiki hii ambaye katika wimbo wake WHEN ameuliza maswali hayohayo.
Anasema akichungulia dirishani anajiuliza mustakabali wa maisha ukoje? Anasema "thinking of the children who are the victims of oppression, beaten donw by war and neaten up by starvation. Let me say. When will this ugly war be over and the children can go out and play? I wanna see. When will all oppressions will be down, and the people will rise up and say, FREEDOM AT LAST, FREEDOM HAS COME".
Nasio anaeleza hamu ya wengi kuanzisha vita kila vingine vinapoonekana kutafutiwa ufumbuzi na pia anaweka madhara ya wazi ya vita akisemana kuuliza "so much bloodshed hate and sorrows, there is no future for the youth of tommorow. So many mothers crying, so many funerals, when will it end?"
Msikilize Nasio katika wimbo huu unaopatikana katika albamu yake ya Universal Cry. Maudhui na midundo yake vyaendana sana.


IJUMAA NJEMA
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

watoto wetu jamani cjui ni nani wa kuwasemea watoto kwani kila mahali wao wanatuhumiwa, wanauwawa, wanapigwa, wanabakwa, sijui twende wapi, sijui tumwombe Mungu yupi wa kukomboa watotoo wetu. inauma sana.

kuna akina sisi tuliokua bila wazazi wakati wako hai, lakini sasa mambo ni magumu sana.nilipambana na wakristo fulani kisa niliandika makala ya kuwatetea watoto wasipigwe, wanarejea andiko la mithari 22;15, nikatamani hata watoto wangeshirikishwa katika kunadika hiyo biblia. inaumma
sasa dini hizo ndizo chanzo cha migogoro yoote ya mauaji. ukiangalia nyma ya ubaguzi wa rangi, kuna dini fulani.

watanzania waliandamana kupinga kuuwawa na kuonewa kwa waisilamu wenzao wa palestina, lakini kawme siio wa Darful, kwa nini?

tunafanya maasi wizi na ujinga kwa jina la dini. marekani akimpiga iraq, tunajidanganya eti imeandikwa. israel ndo baaasi, taifa teule la Mungu. sijui ni mungu yyupi huyo anayemilikiwa na waislaeel na anayewawezesha kuuwa na kutengeneza siraha hatari duniani badara ya kueneza amani, uipendo, mshikamano na umoja! huyo mimi namwita Mungu kichaa kama kweli yupo.

tunachafua uliwmengu eti kwa jina la Mungu. marekani wameandika kwenye pesa zao kwamba, in god they trust, sijui ni mungu yupi wanayemwamini huyu.
ukoloni, utumwa na uuaji, yalifanyika kwa jina la Mungu wa watu fulani. leo Dafur ni kwajina la Mungu fulani japodini moja lakini Mungu anapendelea ngozi fulani zaidi, wapalestina wafwa, kisa? taifa teule la Mungu linataka kurithi mali za duniani. ni mungu yupii anapenda mali za duni kulikoo kuwapenda watu wake? kwa nini Mungu analiwezesha taifa lake teule kuuwa na sio kuokoa na kukomboa watu wake.

ni lazima tumtafute Mungu wa kweli na kueneza ulio ukweli badala ya propaganda za kibanadamu eti mungu anapendlea wajinga fulani wa tifa linalojiona ni lake zaidi.

lazima turudi kwenye msingi wa imani halisi na sio bangi hizi kwa jina la mungu eti

na walilia watotoo, japo ipo siku Mungu wa kweli na mungu wa watu wote na viumbe, atawasikia. ni mungu asiye na taifa wala kabila ni mungu apendaye na kusamehe na kuwakaribisha wote kwake, sio mungu wa kubagua kama tuliye naye sasa

Yasinta Ngonyani said...

Dunia imekwisha ndo maana tunaona migogoro kila sehemu. Yaani hakuna amani kila sehemu vita. Labda ni kweli mwisho wa dunia. Ila ni kweli nakubaliana na Kamala watoto wanapata sana shida wakati hawana hata kosa. Hata imani ile ya kusema kuna Mungu inakwisha maana kila tukiomba hatupati tunachoomba. Kama mzazi na mtu inaniuma sana.

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Kamala nadhani umemaliza hapo. Inasikitisha kuona watu wanamtumia Mungu kukamilisha nia zao. Kutimiza watakayo na kupate wasakacho.
Kila kitu kinatafsiriwa kwa mtazamo wao. Aliyekuwa shujaa leo kesho atakuwa gaidi ama gaidi atakuwa shujaa kwa kuwa tu amebadili mtazamo wake kuhusu wao. Na sie wala hatuulizi, tunaandamana, tunatoa TAARIFA RASMI, na kuunga mkono. Mashujaa wao wanakuwa wetu na sisi tunabaki vibaraka wao. Asiyetujua wala kujua tuishivyo anatupangia nani awe Rafiki na adui yetu kwa kuwa tu amempendezesha ama kumkasirisha yeye.
Hatuwi sisi na hatuna chetu. Sisi ni zaidi ya kivuli chao (sijui kwa kuwa tu-weusi?)
Inakera na kusikitisha. Wakisema nendeni mkaue nasi hatusemi lolote japo twajua kuwa wanaouawa hawana hatia.
Asante Kaka na Ijumaa njema

PASSION4FASHION.TZ said...

Siku zote yanapotokea matatizo kama haya waathirika wakubwa huwa ni wanawake na watoto,baba anaweza kukimbia akaicha familia yake nyuma,lakini mama hawezi popote atakako kimbilia atakwenda na wanae,utakuta mwingine ni mja mzito kukimbia hawezi.

Mimi nasema hivi Tanzania ndio nchi pekee ilikuwa nzuri kwa kuishi lakini inaharibiwa na rushwa,ufisadi ndio vinasababisha watu waone kuwa hapafai lakini ni nchi pekee yenye amani,haya yote tunayaona kwenye TV,tunasikia kwenye redio na kusoma kwenye magazeti namshukuru mungu hayajawahi kutokea kwetu.