Wednesday, March 18, 2009

Hizi zote ni "nafasi za pili"


Ni kweli kuwa NAMNA UONAVYO TATIZO NDILO TATIZO. Na ni kweli kuwa kuwaza si kunena na kunena si kutenda.
Katika maisha yetu tumekutana na "bahati" mbalimbali na baadhi yazo hatukuweza kutilia maanani maana hazikuwa na athari za moja kwa moja kwetu.
Ni kweli pia kuwa katika maisha kuna nyakati ambazo mambo hayaendi kama yanavyostahili lakini pia kunakuwa na nafasi ya KUJIFUNZA KITU NA KUSONGA MBELE.
Hapa ndipo kunapotokea tatizo. Kwamba wawili mwaweza kuwa chini lakini fikra za nini kimewafanya muanguke zaweza kufanana lakini kuwaza juu ya vipi utaweza kuamka na usianguke tena ndipo panapokuwa na mapishano na ndipo DHANA YA KUFANIKIWA NA KUTOFANIKIWA inapokuja.
Hakuna anayekwepa ukweli kuwa kila mmoja anakutana na majaribu, na sidhani kama kuna anayekwepa ukweli kuwa majaribu mengine huja kana kwamba ndio mwisho wa kila kitu kwako, lakini kwa ujumla na undani sivyo. Hiyo inakuwa ngazi ya kupandia kuelekea nafasi ya pili.
Kila mtu ana kile aonacho kuwa amechelewa kukifanya na kujilaumu, lakini ni wachache wenye kukaa chini na kutambua kuwa hali ingekuwa mbaya zaidi kama angechelewa kutambua ama kama ataendelea kung'ang'ania makosa yaliyomfikisha hapo na kushindwa kunyanyuka na kusonga.
Mipango butu katika uchumi nayo yaweza kumfanya mtu ajikute ameishiwa. Na katika mkanganyiko wa uchumi kama sasa ambako wengi wanapunguzwa kazi na kuachishwa, kunaweza kujitokeza lawama na majuto mbalimbali kuhusu maisha yako yaliyopita na namna ambavyo uzembe wa aina fulani umeweza kukufikisha hapo.
Maamuzi fulani fulani maishani yanaweza kuwa yamekufikisha katika nafasi ambayo unaweza kujikuta ukijilaumu na kujijutia zaidi ya kujipanga upya.
Lakini yote ni mipango. Ni sehemu ya maisha. Ni mzunguko wa maisha ya binadamu na ni NAFASI NYINGINE YA KUKUA KIMAISHA. Tumeshuhudia matajiri wengi (akiwemo Donald Trump) ambao "walishachemka" mpaka kufikia kiasi cha ku-file bankruptcy lakini wakajipanga upya na kurejea katika uchumi imara. Na sisi ni vivyo hivyo. Lengo hapa si kurejea na kuwa imara kama wao walivyofanya, lakini kurejea na pengine kusonga zaidi ya tulipokuwa.
Tutambue kuwa watu na maisha vyote vinaweza kutaka kutuamulia namna ya kuishi bila kujua mipango na malengo yetu na kama utaviacha vizidi maisha yako halisi utajikuta ukishindwa kuwafurahisha utakao na hata wewe mwenyewe maana utakuwa mtumwa wa maisha yako mwenyewe. Kumbuka Bill Cosby alisema kuwa "i don't know the key for success, but the key for failure is trying to impress everybody".
Ni mtazamo wa namna tuonavyo tatizo unaoweza kutusaidia katika kulitatua tukijua kuwa kila uangukapo na kutambua kuwa umeanguka, una NAFASI YA PILI kufanya vema zaidi.
Nakuacha naye Freddie McGregor akiwa nao Morgan Heritage katika wimbo huu PICK YOURSELF UP ambao katika kiitikio wanatuasa kutoacha kutenda yale mema tupendayo na kutokatishwa tamaa na yeyote katika harakati zetu na kila tuangukapo basi tuamke na kusonga. Wanasema "so you should never stop. For you to reach the top believe in yourself and keep your head up, let no one tell you, you can't make it. And if you're broken down you should now stand up, reach within yourself and pick yourself up, let no one tell you, you cant make it"
Wasikilize kwa makini na kisha furahia kila nafasi ya ziada upatayo.


JUMATANO NJEMA

1 comment:

Koero Mkundi said...

Hii nimeipenda,

ahsante kwa kutuelimisha kaka Mubelwa.