Wednesday, March 18, 2009

Kunena si kutenda.

Niliwahi kuandika juu ya urafiki. Na najua na kutambua kuwa wengi tunao wale tuwaitao marafiki.
Ninao wachache na wengi kati ya wachache hawa wamenena na wachache kati ya wachache wa wachache hawa wametenda. Juzi nimepokea ujumbe zawadi toka kwa RAFIKI ambaye kwa bahati mbaya nilimkwaza kiasi. Kwa hakika kupata ujumbe huo kulinifariji sana na moja kati ya vilivyoambatana na ujumbe huo ni hii zawadi ambayo imekuwa zaidi ya faraja kwangu.
Asante Ryah, maana hujanena tu, bali umetenda.

No comments: