Wednesday, March 25, 2009

Kwanini kwenye uhitaji ndipo tunapokandamizana?

Nilipotundika maelezo juu ya suala la mtatibu na mgonjwa wakati nikielezea tunavyoweza kuwa sawa na tusiwe sawa kwa jambo na wakati mmoja kutoka pande tofauti, Kaka Fred Katawa akaongeza kisa kilichomsibu / ama kuisibu jamii yake akisema:

Ubinadamu kweli umepungua au kuisha kabisa.Leo nimepata mkasa ulionishtua sana.
Ninauguza mgonjwa na anatumia sindano,nimetafuta mhudumu wa kumchomea sindano nyumbani'nesi'
Dawa anazotumia mgonjwa wangu ni za gharama kubwa kiasi.Leo asuibuhi nesi kaiba dawa za mgonjwa!

Wednesday, 25 March, 2009

Pengine la kutambua ni kuwa ni wengi wanaokumbana na matatizo haya. Jamii inaathirika saaana na ukatili wanaotendewa watu wanapokuwa katika uhitaji. Unakuta mtu akiwa mzima analipia taxi kwa bei ambayo wakati mwingine ni nusu ya anayolipa akiombewa kuwahishwa hospitali akiwa mahututi. Sitazungumza tofauti ya kusafiri na kusafirishwa kwa mwili wako maana hiyo ni hadithi nyingine.

Lakini swali ni kwanini kwenye uhitaji ndipo tunapokandamizana?

1 comment:

Subi Nukta said...

Mubelwa, wakale walisema, 'Kufa kufaana', ama 'Kwako dhiki kwa mwenzio rizki' au 'Ukiona karaha, kwa mwenzio raha' na mwishowe, ukumbuke kuwa kidonda chako ndicho shibe ya nzi.
Watu wamekuwa nzi kudandia kufyonza vidonda vya wenzao badala ya kusaidia kutibu. Penye watu 10 binadamu 1, hizo zilikuwa enzi zile za marehemu Marijani Rajab anatunga ule wimbo uliotuwekea hapa wiki iliyopita, sijui leo angekuwa akitunga wimbo huo huo kama angetumia tarakimu 10 kwa 1...