Friday, March 27, 2009

Them, I & Them. MORGAN HERITAGE......Tell Me How Come

Zamani siasa ilikuwa ni kama huduma kwa jamii, lakini sasa ni kama asemavyo aiitavyo Da Subi "si hasa" yenye "visa na mikasa". Mimi naiita PoliTrix. Si njia ya kuleta unafuu na maendeleo / maisha bora kwa jamii, bali ni kuitumia jamii kupata maisha bora.
Viongozi wa leo hawajishughulishi na maswali yawasumbuayo wananchi bali wanajali MAIGIZO yao Bungeni yenye kurefusha vikao na kuwapatia marupurupu mengi zaidi. Hawaulizi maswali yanayoulizwa na "walio chini" juu ya kisababishacho hasara kwa taifa na ambacho kukichunguza ni hasara nyingine maana kutatumika pesa kubwa na matokeo yake hayatawafikia wananchi wenye HAKI ya kujua.
Jamii ina maswali mengi ambayo nina hakika kuwa VIONGOZI HAWATAKI HATA KUYASIKIA kwa kuwa hawana majibu na hilo ni kwa kuwa hawajishughulishi nayo.
Viongozi wengi:
Hawataki uwaulize kwanini wananunuliwa magari mapya na ya kifahari kila miaka mitano na kutumia mamilioni ya shilingi katika sherehe zisizomfaa mwananchi ilhali vitendea kazi na magari mengi ya zimamoto yana hadhi ya kuwekwa makumbusho (yamezeeka).
Ama kwanini kilimo kilicho UTI WA MGONGO wa Taifa hakipewi msaada unaostahili.
Hawana majibu ya kwanini hali ya kinamama kwenye hospitali inakuwa kama ilivyo sasa.
Hawataki uwaulize gharama za safari zao wanazoongozana na watu lukuki kwa kodi ya mwananchi ilhali manispaa nyingi hazina vitendea kazi vya kukabili majanga yanayoua watu kila kukicha.
Hawataki uwaulize pesa za kodi za wawekezaji zinaenda wapi iwapo uwekezaji wenyewe uko hatarini na ukikabiliwa na matatizo haupati msaada wa kutatua
Tabasamu lao litapotea ukiuliza kwanin thamani ya shilingi yazidi kushuka ilhali gharama za maisha zazidi kupanda kwa wenye kipato cha chini?
Hawataki kuulizwa kuhusu mfumuko wa bei unaomnyonya mwananchi wa chini kila
siku Hawataki kuulizwa mengi ambayo kwa hakika ni wajibu wao ama niseme ndicho kilichowaweka hapo walipo.
Ndio maana leo hii naungana nao Morgan Heritage (Bofya hapa kutembelea tovuti yao)katika kuuliza maswali haya waulizayo kwenye wimbo huu TELL ME HOW COME.
Morgan wanaanza kwa kueleza kuwa kama si Mungu wao, basi wasingekuwa na uwezo wa kuendelea kuishi, kisha wanasema "hebu tuangalie mazingira yatuzungukayo tuone yatokeayo na ndipo wanaishia kuuliza maswali hayo ya tell me how come.
Wasikilize huku ukisoma mashairi yao uelimike

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

6 comments:

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Digna Abrahamu said...

Hili darasa hakika linafikirisha.
hii naona pia ni changamoto kwa vijana, yatupasa sasa tuingie katika siasa kwa wingi ili tudai haki zetu tukiwa humo.

私のブログ (My Blog) said...

Thanks Information

BY :
http://palembang-musi.blogspot.com/

malkiory said...
This comment has been removed by the author.
malkiory said...

Inasikitisha kuona kwamba wanasiasa wanakuwa mbali na watu ambao wemewaweka katika ulaji wa wazi wazi.

Kusema ukweli ipo kazi nzito mbele yetu kuielimishajamii,ninachowaomba kama wanaharakati,tusirudi nyuma kukemea haya maovu kwa njia yeyote ile,uwezekano upo kabisa wa kuwafikishia ujumbe kwa walengwa.

Ninayo imani kuwa taifa letu litajengwa na wachache wenye moyo na wenye uchungu nalo