Monday, March 30, 2009

Za Kale vs Maisha ya sasa. USIA KWA WATOTO, TUPATUPA

Baadhi ya wasanii wa Juwata Jazz Band. Watatu waliosimama toka kushoto (kwao) ni Joseph Maina, Tx Moshi William na Athuman Momba ambao wote sasa ni marehemu. Lakini ujumbe wao utadumu milele
Sina hakina ni wangapi walibahatika kupata nafasi ya kuusiwa na wazazi wao kuhusu mabadiliko ya maisha kulingana na nyakati mbili (ujana wa wazazi na wetu sisi). Ni ukweli kuwa kuna mabadiliko meengi ya kimaisha kuanzia thamani ya pesa mpaka, matumizi yake, umuhimu wa kuweka akiba na mengine mengi.
Pengine huwa tunausiwa lakini si kwa kuongea kama BABA/ MAMA NA MWANA, bali mara nyingi ni wakati wa kugomezwa na kufokewa.
Lakini pia si wengi ambao katika hali ya kirafiki wanaweza kueleza matatizo wanayopitia kwa kuwa walishindwa kuwa na umiliki mzuri wa pesa zao. Ni CHANGAMOTOYETU sote kuweka malengo mema na kuelekeza mabadiliko ya maisha kwa wale watutegemeao.
Leo hii tunao JUWATA JAZZ BAND (ambao sasa wanafahamika kama Msondo Ngoma Music Band) ambao wanakuja na nyimbo zao mbili kuhusu umuhimu wa kupanga vema matumizi. Wa kwanza ni Usia kwa watoto na wa pili ni Tupatupa ambao ni juu ya kijana anayejutia matumizi yake mabaya ya pesa.
Sikiliza, burudika na jifunze.

Kisha TUPATUPA

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

No comments: