Saturday, April 4, 2009

CHANGAMOTO CHANGAMOTONI

Ni kweli kuwa Blog hii iko changamotoni. Kitendea kazi chake kimechangamotolewa na changamoto ya kirusi na sasa hakiko kwenye hali njema kimaisha. Lakini kirusi hiki chatibika na sasa kitendea kazi kiko matibabuni.
Twaamini kitarejea punde na kuendelea kuwakilisha na kuwasilisha.
Pamoja daima

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Naamini kuwa utarejea karibuni na kila kitu kitakuwa shwari. Nategemea kila kitu kitaenda safi na utakuwa nasi karibuni.
TUPO PAMOJA

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Laptop yangu pia imekufa kabisa. Sijui ni mnyoo wa Conficker ama nini sielewi. Ni mali ya chuo na kesho naipeleka wakanibadilishie. Kwa vile mafaili yangu yote yako salama si neno.

Koero Mkundi said...

Pole sana kaka Mubelwa.
Naamini kuwa utarejea na kufidia yale tunayoyakosa katika kipindi hiki cha kitendea kazi kuchangamotoliwa....

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

"...kitendea kazi kuchangamotoliwa" Koero, Kiswahili kimeswahilika hasa!

Anonymous said...

Ni kweli changamoto inaweza kuwa changamotoni. Challenging a challenge, lakini changamoto kuchangamotiwa ni kiswahili kipya. Lakini natumaini tayari tatizo la kirusi linatatulika na utakwa hewani, naona ni bora kuendelea kutupa changamoto za maisha, uwe na amani