Saturday, April 11, 2009

HERI YA PASAKA

PASAKA yatambulika kama moja ya siku muhimu katika maisha ya MKRISTO. Siku ikamilishayo utimilifu wa ukombozi wa mwanadamu kutoka kwa Yesu Kristo. Ni ukombozi uliotokana na MSAMAHA WA DHAMBI ambao umekuwa ukisherehekewa kwa takribani miaka 2000 sasa. Basi nasi Changamoto Yetu Blog tunawatakia PASAKA NJEMA na kukumbushana kuwa kama ukombozi huu tunaousherehekea ni kwa msamaha wa dhambi, basi nasi tukumbuke kutenda hayo ili kupeana ukombozi halisi baina yetu na ndani mwetu.
Tuianze kalenda yetu ya mwaka (kama tuianzavyo kila siku) kwa mipango mipya ya kutowakwaza wenzetu (pale tuwezapo) na pia kusamehe (pale iwezekanapo) ili kuweza kuwekana huru na kuishi kama tutakiwavyo.
ONE LOVE, ONE AIM, ONE DESTINY
Tuungane na Luciano katika wimbo Forgive Them Lord kutoka katika albamu yake Upright
PASAKA NJEMA

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

HERI YA PASAKA NAWE PIA ila usile mayai mengi:-)

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahahahaaaa. Asante saana Dadangu. Heshima, Upendo na Baraka kwako na kwa familia. Nawaombea kila lililo jema katika maisha mema muishiyo.
Blessings

Anonymous said...

nuff nuff respect man.

www.ringojr.wordpress.com

Fadhy Mtanga said...

Pasaka njema kwa wanablog wote.

Mary Damian said...

Pasaka njema, Neema ya Mungu isikupungukie!

Koero Mkundi said...

Nimekuona mzee..