Majira ya joto yameanza sehemu nyingi na hapana shaka tutaanza kutambua kuwa kuna JUMUIYA nyingi za waTanzania sehemu mbalimbali. Niliwahi kuuliza kuwa hizi jumuiya ni za nini na za nani? (bofya hapa kusoma). Nia ilikuwa kujiuliza maana halisi ya hizi Jumuiya ambazo zimegeuzwa kama vyama vya Kufa na kuzikana na sherehe za majira ya joto. Ninaamini kuna mengi ya kutenda ndani ya jumuiya zetu lakini mara zote tumezishuhudia zikiibuka nyakati za sherehe, misiba na ziara za viongozi.
Sina shaka kuwa sasa ni wakati muafaka wa kuanza kuziona zikiibuka na kuandaa ma-BASH mengi ya kutumbua pesa bila kujali uhitaji na kukumbushana mengi muhimu ya kutenda baina ya wanajumuiya.
Naamini wenye macho wataona haya yanenwayo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Nasikia hata kwenye hayo "ma-bash" mambo ni yale yale ya ulimbukeni: Nani mwenye gari la bei mbaya zaidi, nani aliyepiga pamba kuliko mwingine....na mambo mengine ya ajabu ajabu. Jamaa mmoja alihudhuria "bash" moja kule H Town na alisema kwamba mambo aliyoyaona huko yalimshangaza. Pengine si jambo baya kwa watu kujirusha na kuonyesha ufanisi wao.
Jumuia hizi zingemakinikia mambo ya kimaendeleo zingesaidia sana. Kwa nini, kwa mfano, zisijikite katika kutafuta pesa za kusaidia mayatima kule nyumbani? Au kukusanya vitabu na kuvipeleka katika mashule ya kata? Au vifaa vya mahospitalini...au.....
Post a Comment