Wednesday, May 6, 2009

Changamoto Yetu yaenda shambani

Ni wakati wa kupanda. Kupanda nikitegemea kuvuna wiki mbili zijazo. Ni kupanda huku ambako kutanilazimu kuwa mbali kiasi na mji wangu wa blogu na kuwa katika shamba niendalo kupanda na ambako ninaamini kuwa kama ilivyo kwa wanachama wa DECI waliokuwa "wakipanda" pesa na "kuvuna" baada ya muda, nami mavuno yangu yatakuwa ndani ya wiki mbili.
Ndani ya wiki hizi mbili nitakuwa napatikana lakini si kwa "mwendokasi" niliozoeleka. Naamini nitarejea kwa nguvu zote mara baada ya kumaliza Mavuno yangu wiki mbili zijazo.
Hata hivyo, bado nataraji kuwa na muda wa kupita na kujuza machache kila nipatapo nafasi (hapa na kwenye majamvi mengine), na pia habari zilizo kwenye "foleni" zitaendelea kuingia hapa kibarazani kama kawaida.
Pamoja Daima
Mpaka wakati huo.......Stay focus

7 comments:

Anonymous said...

Kazi njema na uache unyapara huko shambani, ufanye kazi kikweli kweli uwe mfano wa kuigwa!
Unapanda mbegu za mazao gani shambani?

Simon Kitururu said...

Kila la Kheri Mkuu!

Yasinta Ngonyani said...

Nami nakutakia kazi njema pia nasema kama Da Subi ufanye kazi kweli si kuwa nyapara tu.

Fadhy Mtanga said...

Kupanda? Kisha kuvuna baada ya wiki mbili?
Kila la kheri mkuu.

Sophie B. said...

Kazi njema!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kapande kwa uangalifu na hali ya hewa ikuunge mkono. Itunze vizuri mimea itakayochipuka ili mavuno yawe mengi. Jamii nzima inasubiri kufurahi pamoja nawe! (Mlimaji mmoja, lakini walaji wengi)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ni vyema na haki. hivi sasa ni mvua za masika zinamalizia kunyesha kwa hiyo utavuna kwa sana.


shumaalamu waitu