Friday, May 8, 2009

Them,I &Them. NASIO .....Dangerous

"I heard your speeches, man and your empty promises. But now that i know, YOUR WORDS ARE DANGEROUS"
" I see so many innocent begging for the guilty, but the blind is the victim in the land of evil sighted. Where there's no vision, man the people suffer, see them cornered by their judgements, and they're consumed by their hatred."
Hili ndilo nilionalo katika "mipasho" ya Mengi na Rostam Aziz. Wamekwepa ukweli. Wanaahidi kutoa maelezo ambayo hayajibu tuhuma halisi na hayafafanui kama kuna kuhusishwa na ufisadi. Hapa ni mchezo wa "gotcha" ambao ni kunyoosheana vidole na kukwepa ukweli. Kibaya zaidi ni kuwa Watanzania wanaendelea kufurahia tuu "wanavyoumbuana" bila kujua kuwa wakati wa kuumbuana ukiisha, hakuna atakayekuwa na la kujibu maana watakuwa wamehamisha mada toka kwenye ufisadi kwenda kwenye nani alifanya nini na anamiliki nini na hicho amilikicho kilifanya nini na kushirikiana na nani. Lakini hakutakuwa na suala kuu.
Lakini pia yapaswa kujiuliza kuwa kama hawa wanayajua yote, na kama wana ushahidi kiasi cha kuyasema mbele za waandishi wa habari, i-wapi serikali yenye dhamana hiyo? Ni kweli kuwa hawa wamepata "data" hizi mahala ambapo serikali haiwezi kuzipata? Ni kweli kuwa Mengi na Rostam na hao wengine wanne ndio walioifilishi nchi? Peke yao? Mbona hatuambiwi zilikofia Kagera Retco na RETCOs nyingine? Kuna mengi ya kusafisha na kibaya ni kuwa waliohusika ndio kizazi kilichopo madarakani sasa na kuisafisha Tanzania ni pamoja na kupanua jela maana wahusika wa ufisadi halisi unaoifilizi nchi ni wengi, walianza zamani, wamajilimbikizia mengi na wote wanahitaji kwenda jela. Sijui ni nani atakayewafunga maana hata "wafungaji" ni wahusika. Mmhhhhhhhhhhh??!!!!?!?!!?
Ndio maana napenda sehemu hii ya wimbo wa Nasio anaposema "don't worry about the pretty things you hear them say"
Msikilize Nasio Ijumaa ya leo akisema DANGEROUS.

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

mumyhery said...

kaaazi kweli kweli

Yasinta Ngonyani said...

Ijumaa njema nami nasema kaziiiiiii kwelikweliiii Lol