Tarehe kama ya leo miaka uijuayo wewe Dadangu ilikuwa ni baraka ndani ya familia ya Mama Namsifu na Baba Japhet Mkundi. Ni kwa kuwa ulizaliwa. Lakini kuzaliwa pekee si kitu kilichokufanya kuwa wa muhimu kama ulivyo, bali ni malezi toka kwa wazazi na namna ulivyoyapokea. Ni kwa hili ninapopenda kusema SHUKRANI KWA WAZAZI kwa namna walivyokulea na kukupa uwezo wa kuwa ulivyo.
Nasi sasa tunaweza kufaidi malezi yao kwa kusoma mengi uandikayo kwenye "baraza" lako pamoja na sehemu utoazo maoni.
Binafsi nina mengi ya kujivunia kuhusu wewe. Tunawasiliana, tunajuliana hali, tunashauriana na pia kufurahia kufamiana kwa familia zetu.
Napenda kukueleza kuwa unapendwa, unaheshimiwa, unathaminiwa na pia kutakiwa kila lililo jema katika mwaka mpya uuanzao sasa.
Shukrani kwa kila aliyekuwezesha kuwa ulivyo, na pia kwa kila unayeshirikana naye katika kuzifanya siku tuishizo kuwa za mafanikio kwetu.
Happy Birthdate K.
We owe nobody NOTHING BUT LOVE.
Luv You Sis
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Hongera sana kwa siku hii muhimu kwako mdogo wangu. Uwe na siku njema.
Kila la kheri katika mwaka mpya uuanzao. Ubarikiwe ktk kila jambo ulifanyalo.
Hizi suprise nyingine ni za kushangaza, unajua hata sikumbuki siku yangu ya kuzaliwa!!!!
ha ha ha ha haaaa!!!!
Juzi ilikuwa nisafiri kwenda Arusha, ilikuwa ni safari yab ghafla ambayo mzee Mkundi alinishitukiza, basi kwa akili yangu nikajua sherehe ya kuzaliwa kwangu nitaifanyia Arusha,nikampigia dada yangu asimwe simu na kuhabarisha ujio wangu na kuhusu sherehe ya kuzaliwa kwangu, bila hiyana dada yangu Asimwe akaandaa keki na vikorombwezo vingine.....
Lahaulaaa safari ya arusha ikaota mbawa, yaani hata sikukumbuka kuwaambia wasomaji wa VUKNI kwamba jana ilikuwa ndio siku ile mama Namsifu alipomzaa Koero...
Nasikitika kwamba Asimwe kaila keki ile peke yake......hurumaaaa.....
Jana nilitoka na mashoga zangu tukaenda zetu Sea Cliff Hotel kuchapa umbeya....bna siku ikapita.
Ahsante sana kaka Mubelwa kwa kunikumbuka, pamoja na wadau wote mliotoa salam za kunitakia kila la heri......Koero ndie mimi na jana nimetimiza umri wa miaka 24.....
mnashangaa nini? ukeli ndio huo....karbuni san VUKANI
Post a Comment