Sunday, May 10, 2009

Kwa kinamama wema wote. ASANTENI

Nimelelewa na kinamama wengi. Nasema kinamama kwa kuwa hata kinababa walionilea wanasema walilelewa na kinamama. Naamini sehemu ya malezi yao ndio iliyowafanya wawe walivyokuwa na kunisaidia kuwa nilivyo. Lakini pia nimelelewa na Dada zangu, Mama, Shangazi, Bibi na wengine ambao kwa namna moja ama nyingine wamechukua jukumu la U-MAMA kunifanya niwe nilivyo. Nami naendeleza mema niliyotendewa kwa wengine ambao naamini watapitisha haya.
Siku ya leo ni siku ya kuwaenzi wote. Kukumbuka na kutukuza yale yaliyofanywa, yanayofanywa na pia yanayowakwaza kuendelea kufanya yale tuliyofanyiwa ama ambayo tunatamani kufanyiwa.
Bado kuna mengi kuhusu kinamama yaliyosahaulika. Na hapa sizungumzii nafasi za upendeleo wanazoonekana kufikiriwa, bali nazungumzia madhara na athari zinazoonekana kuwakumba kila mara yajapo magonjwa na hata vita. Mitetereko yote ya maisha yaonekana kuwakumba kinamama zaidi na ni wachache wakumbukao kuwatetea na kutaka uwepo wa haki kwao.
Nakumbuka mmoja wao ni Lucky Dube ambaye katika wimbo wake GOD BLESS THE WOMEN alisema We, praise heroes everyday, but there are those that we forget To praise
The women of this world. They don't run from anything. They stand and fight for what's right.

Twawashukuru saana kwa msimamo wenu mwema na katika siku kama ya leo tunatoa muda maalum kuadhimisha harakati zenu, na kwa siku zetu zote maishani, TUTAWAPENDA DAIMA
ASANTENI


In the middle of the night I heard her pray so bitterly
And so softly yeah...
She prayed for her children
She prayed for their education,
Then she prayed for the man
That left her with her children.
We, praise heroes everyday
But there are those that we forget To praise
The women of this world.
They don't run from anything
They stand and fight for what's right

Chorus
Oh oh oh...
God bless the women

Even when times are so hard
They are so cool, calm and collected.
They don't run from anything,
They stand and fight
For what is right

They do not run from responsibilities
They stand and fight for what Is right

Chorus till fade...

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Asante kwa kututhamini na kutuenzi kina mama/dada nk

mumyhery said...

Nikiwa mmoja wao naomba niseme SHUKRANN!!!

Fadhy Mtanga said...

God Bless The Woman!

Mija Shija Sayi said...

Ubarikiwe sana, tunashukuru kwa kutupa maneno yenye faraja. ASANTE.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

labda bi kweli japo wapo wachukiao kuzaliwa na wanawake. je yupi mmoja wao?

Anonymous said...

whose song is this? what a great words..