Wednesday, May 13, 2009

Ni maamuzi ya sekunde kadhaa yatuathiriyo milele

Kuna wakati tunaopumbazwa na namna tukutanavyo na matatizo na hata namna ambavyo tunapitia athari zake. Pengine twapumbazwa na kudharau ATHARI HALISI za maovu yetu na kung'ang'ania zile ambazo zinatokea papo kwa hapo. Kuna ukweli kuwa athari mbaya zaidi ni zile zinazochukua muda kujitokeza na ambazo huchukua muda "kuzikarabati" japo zaweza kuwa zimesababishwa na tukio lililochukua muda mfupi kulitenda. Nchi inakuwa maskini kwa kuwa kuna waliochukua sekunde chache kusaini mikataba mibovu, watoto wanaathiriwa kisaikolojia kwa kuwa kuna aliyechukua dakika chache kuwabaka na kuwalawiti. Baadhi ya watu wanaugua miaka na kuitesa jamii kwa kuwa kuna ambao hawakuwa makini katika kudhibiti mihemko ya miili yao kwa dakika chache. Maelfu wanateketea kwa kuwa kuna anayefanya maamuzi ya sekunde kadhaa kutangaza vita. Na japo hatuoni athari zake kuu papo kwa hapo, huwa zinakuja. Lucky Dube aliimba kuwa "the things you say and do today, will come and hunt you tomorrow"
Wiki hii kwa mara nyingine kumetokea mauaji ya wanajeshi wa kimarekani ambao wameuawa na mwenzao katika hospitali ya kushughulikia watu walio na msongo wa mawazo (stress). Na licha ya kuwa yajulikana athari wanazopitia wanajeshi hawa kisaikolojia, bado kuna kupuuzwa kwa kusitishwa kwa vita ambavyo vyaonekana kuwaathiri zaidi.Waweza kuisoma habari yake kwa kubofya hapa. Niliwahi kusikiliza habari za askari ambaye kabla hajajiua alieleza namna alivyokuwa "akiwindwa" na picha za aliyotenda kwa wale asio na hakika kama walikuwa na hatia. Na ndio maana tuliwahi kuandika katika kipengele cha I & THEM juu ya stress ambazo aliwahi kuziimba Lucky Dube alipojiweka katika nafasi ya askari aliyerejea nyumbani kutoka vitani. Pengine nirejeshe wimbo na maneno yake kuweza kujua kile ambachi kilifunikwa kwa viongozi wetu kilifunuliwa kwake. Ukiusikiliza wimbo na kusoma hiyo habari, waweza kutambua wanayopitia wenzetu hawa katika hivi vita wanavyotumbukizwa na kujikuta wakijiwekea athari nyingi akilini mwao




Stand for the truth you stand alone
government will cover up

I saw a man sitting in a room
holding a gun to his head,
he said man oh man
what am I gonna do
I can't change the past but I can change the future
If I pull this trigger right now, right here
everything will be over
not a day goes by I don't see them in my dreams
not a day goes by I don't hear them screaming in my ears
begging for mercy, pleading innocent
since my heart is made up to be as cold
as the barrel of this gun I hold
I would pull the trigger anyway

chorus
I was a soldier, following instructions from a man
we have known as the general

Stand for the truth you stand alone
Government will cover up

So many medals, so many praises
nothing can take away the guilt
that I feel inside me
Government covered up every crime we committed
against humankind
not a day goes by, I don't see them in my dreams
not a day goes by, I don't hear them crying in my ears

Chorus
I was a soldier, following instructions from a man
we have known as the general

Stand for the truth you stand alone
Government will cover up.

2 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kaka, umenifikirisha sana. Nimeketi na kuukumbuka huu wimbo wa Lucky Dube na kunikumbusha pia mambo mengi yanayosababishwa na maamuzi mabovu ya wachaguliwa na wananchi, kama wanavyojiita.
Ni hayo tu!

Putri Erdisa Januarti said...

hey! thanks for blogwalking.. :D
i've said that i wanna copy your subtitle up there, but i just forgot to! lol. so thanks God you contact me again. :D

anyway, what language is it? I hope i could understand what you are talking about! :)

have a blessed day too.