Kuna maasi ambayo yanaendelea kuisumbua dunia yetu ambayo mpaka sasa wengi hawajajiuliza ni kwanini yametokea, ni kwanini yapo na ni kwa manufaa ya nani?
Vita vinaendelea "kuimung'unya" Afrika yetu na cha kusikitisha wanaendelea kuumia zaidi ni kinamama na watoto. Kwa kuwa vimeshatokea na kwa kuwa hakuna suluhisho la hakika wakati vita vinaendelea, naishia kujiuliza swali alilojiuliza Nasio Fontaine anapojiuliza akisema "i'm wondering what the future will be? Thinking of the children who are the victims of the oppression, beaten down by war and eaten out by starvation. Let me say, when will this ugly war be over and children can go out and play? I wanna see. When will all the oppression will be gone, and the people will rise up and say, FREEDOM AT LAST"
Na anaendelea kueleza mengi kuhusu kinamama na watoto akisema "so much bloodshed, hates and sorrows, there's no future for the youth of tomorrow. SO MANY MOTHERS CRYING, so many funerals, when will it end?"
Nami najikuta nikijiuliza maswali mengi pasipo majibu. Ni nini hasa sababu ya vita? Ni kwa ajili ya nani? Vyamnufaisha nani na kumuumiza zaidi nani?
Msikilize NASIO FONTAINE katika kibao hiki When kilichomo katika albamu yake UNIVERSAL CRY**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
5 comments:
Ahsante kwa ujumbe mzuri kaka Mubelwa.
Peace Respect.....
Sababu kubwa ya vita hasa Africa ni uroho wa mali na madaraka.
Lakini chanzo halisi ni brain-wash kutoka kwa watengenezaji wa silaha, ambao wanapanda chuki kwa watu na kuzua mizozo, na hapo wanapata soko kubwa la silaha kwa manufaa yao. Utaona vita nyingi zinatokea sehemu zenye utajiri wa asili kama madini, mafuta nk. Malipo ufanyika kwa pesa taslimu au kupeleka bidhaa hizo hukoo kwa mtindo wa barter trade. Unapewa silaha kwa kutoa malighafi.
Inasikitisha kuona akina mama na watoto ambao hawafaidiki na dhumuni la vita ndio wanaokuwa waathirika wakubwa.
Asante kwa kunijulia hali Da Koero. Nuff Respect Empress.
Ndg Chid. Heshima na Upendo kwako. Karibu changamotoni na kwa hakika nafurahi kuifahamu "darubini" yako na najivunia kuwa nawe hapa.
Blessings
Nasikia lakini Mungu wa ashindaye vita anaombwa pia na waathirikao na vita!
Namwomba mungu awape watu wote hapa duniani amani kwani inahuzunisha sana. Ijumaa njema nawe pia Mzee wa Changamoto
Post a Comment