Sunday, June 21, 2009

Happy Father's Day.......GOOD PAPA(s)

image from www.holidayjoys.com
"Role modeling is the most basic responsibility of parents. Parents are handing life's scripts to their children, scripts that in all likelihood will be acted out for the rest of the childrens' lives."--

Stephen R. Covey
Siku kama ya leo kila mwaka huadhimishwa kuwakumbuka, kuwashukuru, kuwaheshimu na kuthamini mchango wao katika maisha ya wengi. Nami nachukua nafasi hii kumshukuru na kumuombea Baba yangu mpendwa ambaye amekuwa na bado ni ROLE MODEL wangu maishani. Lakini pia najua kuwa Babangu amekuwa alivyo na amenilea kwa misingi myema kwa kuwa alilelewa vema na Babake. Wako wengi ambao wana wazazi japo wazazi hao hawaonekani kuwa na msaada kwa maisha yao, lakini wapo wazazi ambao walitumia muda wao mwingi "kuwekeza" katika maisha ya watoto wao na sasa wametangulia mbele ya haki lakini wametuachia HAZINA kubwa ya busara na maisha mema.
Nami leo napenda kuungana na ndugu wote ambao walipata malezi bora na mema toka kwa Baba zao lakini kwa mapenzi ya Mungu wametangulia mbele za haki. Hawa wana kila sababu ya kukumbukwa na kuenziwa na leo napenda kuungana na Luciano katika kuwakumbuka, kuwaombea na kuahidi kuendeleza mema yote waliyotufunza kupitia wengine.
Msikilize aliloambiwa Luciano asemapo "what you make out of life, he said, depends on what you put-in, my child". Ndio usia alioupata toka kwa Babake na naamini wengi wameambiwa haya.
Na tuwakumbuke na kuwaenzi kinababa ambao wanatupenda na kuwekeza kwetu. Na wimbo huu ujao ni wazazi ambao walitupenda saaana, wakawekeza saaana na kisha wakamaliza kazi na kutangulia mbele ya haki. Ni GOOD PAPA toka kwake LUCIANO.

NB: Ninalojifunza toka kwa Luciano ni kuwa haijalishi BABA alikuwa na maisha ya kiwango gani, bali amefanya nini maishani. Changamoto yetu hapa ni kujiuliza kuwa tunawaenzi vipi kinaBaba zetu na kwa sisi Baba watarajiwa tunajiandaa vipi kuwalea wanetu?
JUMAPILI NJEMA

5 comments:

Anonymous said...

Heri kwa sikukuu ya Baba!
Baba waliopita, waliopo na wanaotarajia kuwa Baba, hongereni kwa kumudu majukumu ya malezi na utunzaji wa familia. Baba mwenye busara njema hujenga na kuweka msingi kwa ajili ya familia yenye busara njema!
Heri kwa sikukuu ya Baba!

Yasinta Ngonyani said...

Nami nasema heri sana kwa sikuu ya akina baba wote duniani

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duh! kumbe na mibaba inasikuyao? huonekana kuwa minyanyasaji ya wamama na watoto tu!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Maneno ya busara hayo dada Subi. Hongereni akina baba - Kamala - na wengineo! Na Mzee wa Changamoto bado tunakusubiri kama bado huwaja baba!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

matondo, sijui kama mimi ni baba au?