Tuesday, June 30, 2009

Uzee ni nini na mzee ni nani?????

Kwani nikivaa hivi nahesabika mzee?
Nimekuwa nikisikia maneno na misemo kama "Huyu mzee" ama "Ana mawazo ya kisee" ama "Anafanya mambo yake kizee"
Naendelea kujiuliza hivi UZEE NI NINI?
Mvi, mavazi, muonekano, mihangaiko ama?
Nisaidie

5 comments:

Anonymous said...

Mzee/Uzee ni Mubelwa B kwa kuwa anajiita 'Mzee wa Changamoto'.
Uzee ni hali ya kuwa na umri mkubwa kulingana na ufafanuzi wa umri wa jamii husika.
Mzee ni jina linalotumika kwa lugha ya kisasa kumaanisha au kutambulisha mtu mwenye ukwasi, yaani utajiri wa mali, fedha, cheo nk.
Umependeza kwenye picha kwa mavazi yako na maringo yako ya mkono kidevuni.

Yasinta Ngonyani said...

Uzee ni wewe mwenyewe kama umeamua kuwa ni mzee basi utajiona mzee. Naona da Subi amesema yote lol!!!

Simon Kitururu said...

UZEE na MZEE yote ni maneno tu !

Kwa mtazamo mwingine MZEE ni MTOTO kwakuwa Mambo ya Aitwaye Mzee SANA ni sawa na ya MTOTO SANA kwakuwa wote ujanja wao UNAHITAJI nepi!

Mzee ni mtaalamu au anakutisha kwa BUSARA na uzoefu au tu ngawirana pesa kama anakulipa mshahara .

UZEE nukuu ule wimbo:

Watoto wangu eeh
Sinanguvu tena!
Ya kuua simba
Na SIMBA ni mkali.....

Unaukumbuka?:-)

Mbele said...

Watu kule nyumbani ni wabunifu sana katika matumizi ya lugha. Leo utasikia mtuhumiwa wa ufisadi anaitwa "mzee wa vijisenti" :-)

Mzee wa Changamoto said...

Dot seventy seven, nashukuru kwa "credit" za "pozi". Si unajua hizi ni zileee enzi za bugaluuuu!!!? Hahahahaaaa. Nashukuru pia kwa msaada wa tafsiri ya Uzee. Dada Yasinta asante saana kwa kutufanya tujiangalie wenyewe tunapotafsiri vitu. Kama Mkodo wewe ndio umeturejesha mawazoni kabisaaaa. Kuwa kama mzunguko ni nyuzi 360, basi baada ya 350 tunarejea kwenye mwanzo na hapo kunakuwa na mstari mwembamba kati ya mtoto na mzee.
Profesa. Heshima kwako. Ni kweli kuwa nyumbani wanakuwa "wabunifu" katika matumizi ya maneno, japo sina hakika kama wanabuni vitu ili kutuendeleza. Ni kama "kukata ukali wa maneno" ili wasiitwe wezi.
Lakini zote ni changamoto kwangu na jamii yetu.
Mbarikiwe saana