Tuesday, June 30, 2009

Kaka Bwaya, u-wapi?

Picha toka Jielewe (bila idhini) Lol
Ni zaidi ya mwezi sasa tangu umetundika m-jielewesho katika blogu yetu ya JIELEWE na sijabahatika kukutana na maoni yako wala taarifa za kupotea kwako Mkuu. Ni mihangaiko yetu ya kila siku? Ama ni safari ambazo wakati mwingine zakupeleka kusiko na vitendea kazi? Kuna aliyewahi kuniambia kuwa huzuni ya sasa ni wekezo la furaha ya baadae. Nasi twasubiri utakayorejea nayo huko uliko
Popote ulipo natumai utakuwa mwema na unakamilisha na kutimiza malengo na mipango uliyonayo na tunakutarajia JIELEWEni hivi karibuni.
Amani kwako

3 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

labda alikuwa ndani ya ndege moja wapo iliyokarashi!!!!!!!!!!!

jiandae kuheki ili urith blogu yake.

(kama bado yuko hai nitajuuuta kuyasema haya)

Anonymous said...

Kamala - you make me happy ALWAYS with your comments! Keep it up!

Christian Bwaya said...

Ha ha ha haaa! Nimejitokeza kabla blogu haijarithiwa!

Nimerejea wapenzi. Kuna uzembe niliufanya ndege ikakrash. Nikiri hilo. Uzembe wenyewe ulinifanya nisiweze kupangilia muda wangu vizuri. Matokeo yake eeeh ikawa kila siku nikawa nikijiahidi kuandika kesho. Na kesho yenyewe haikuwahi kufika mpaka leo.

Nawashukuru kaka Mube na Kamala. Nimerejea. Naamini ndege haitakrash tena. Tuko pamoja.


@Kamala, wakati wa kuona mimi na wewe umekaribia. Uso kwa uso hivi karibuni.