Monday, June 29, 2009

Za Kale vs Maisha ya Sasa.....KIFO

Hakuna atakayeweza kubisha ukweli kuwa wiki iliyomalizika jana imekumbukwa kwa matukio ya kupoteza watu wenye mvuto na vyombo vya habari. Nasema MVUTO KWA VYOMBO VYA HABARI kwa kuwa naamini kila mtu ni muhimu na kila mtu ana nafasi kubwa kwa watu na jamii husika, bali baadhi wanakuwa na kazi ama maisha ambayo yanawagusa wengi, kwa namna nyingi na matokeo yake ni kutambuliwa mbele ya wengi.
Wiki hii kumekuwa na matukio ya kufariki kwa watu waliotambulika katika nyanja ya mawasiliano na wengi wao wameondoka katika hali inayoweza kuitwa "ghafla." Nazungumzia watu kama Prof Haroub Othman, Sheikh Suleiman Gorogosi, Michael Jackson na hata Bill Mays ambao wote wameondoka usingizini. Vifo vyote vimeaacha wengi wakiuliza vinatokeaje ama vinakujaje ama dalili na wengine kuuliza "kwanini hawa tuwapendao?"
Ndio swali alilouliza Dr Remmy katika wimbo wake huu kuhusu KIFO. Maswali aliyouliza Remmy mengi yanaendelea kuulizwa juu ya vifo hivi vya wiki iliyomalizika jana na bado swali la kale laendelea kuulizwa katika maisha ya sasa.
Buriani kwa ndugu nasi jamaa wote kwa haya yaendeleayo kutukumba.

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

3 comments:

Born 2 Suffer said...

Kweli kifo hakina huruma wengine wanakitafuta na wengine kinawaijia bila kupenda, Mzee remmy kaishia wapi siku hizi?

Simon Kitururu said...

Kifo nishai kama hunampango wa KUJIUA.:-(

Yasinta Ngonyani said...

HAhahahahaha nashindwa kuacha kufurahi yaani huu wimbo nausikiliza kila siku asante sana kwa kuuweka hapa. Dk. Remmy ni familia yeyu hapa kwetu yaani anapendwa na nyumba nzima.