Sunday, June 28, 2009

BURIANI Prof HAROUB OTHMAN

Nimpokea kwa masikitiko taarifa za Prof Haroub Othman.
Profesa alikuwa mmoja wa watu waliokuwa mstari wa mbele kujitokeza na kuonesha msimamo wake huku akiueleza kiuchambuzi kuhusu mambo mbalimbali. Lakini kama ilivyoripotiwa na vyombo mbalimbali, amefariki akiwa usingizini.
Pumziko la milele upate na shukrani kwa kazi kubwa ya uelimishaji wa umma kwa njia ya darasa na vyombo vya habari ambao umeufanya kabla ya kukutwa na mauti.
Pole kwa wanandugu na jamii yote.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Marehemu astarehe kwa amani peponi amina.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Dah! Prof. Haroub Othman alinifundisha pale Mlimani. Alikuwa mmoja kati ya maprofesa wazuri kabisa na wachambuzi makini wa masuala ya kisiasa na maendeleo na alijulikana Afrika na ulimwenguni kote. Hili ni pigo kubwa. Mungu ampe pumziko jema!

malkiory said...

Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Mimi pia alinifundisha Mliman Development studies hasa kwenye mada ya Civil society.

Ilikuwa ni wiki ya kipekee, ukizingatia kuwa ni mfululizo wa vifo vya watu mashuhuri. Ukianzia kwa Michael Jackson, Horoub Athman na Sheh. Gorogosi. Lakini yote ni mipango ya mungu sisi binadamu hatujui makusudi yake.