Thursday, July 23, 2009

ADHABU: Changia kuhusu adhabu hii

Tumekuwa na mazungumzo ya mara kwa mara kuhusu adhabu na katika makala moja iliyoandikwa na Da Yasinta nilizungumza kuwa bado nakubali kuwa viboko vinatakiwa kuendelea japo nakubali kuwa kuna haja ya kudhibiti viboko kama onyo na si kukomoa. Na leo nimeletewa hii na Dada Subi anayehitaji tuungane kuijadili hii.
Msome na kuchangia tafadhali.

Sikatai kwa asilimia 100 kuchapa mtoto kiboko cha maonyo, lakini inapofikia hatua kama hii, kweli kuonya kwa kiboko ni fundisho ama ni ukatili?
Huyu ni mtoto wa kike, amechapwa na mwalimu wake wa kiume, ni katika Sekondari moja huko Iringa, imetokea jana July 22, 2009, mtoto akaogopa kwenda polisi au hospitali kwa kuhofia kwa mwalimu atamwadhibu zaidi. Aliyenitumia picha hii anasema kisa cha kuchapwa hivi ni hasira iliyojificha kwa mwalimu huyo kwa kushindwa kutimiza azma yake nyingine toka kwa binti huyu.
Nimetumiwa picha hii toka Iringa, aliyenitumia hajajua jambo muafaka la kufanya, naomba kuweka kwenu ili watu wajadili na kutoa mapendekezo kipi kifanyike kuhusiana na hali hii.
Mapendekezo yenu nitayafikisha kwa aliyenitumia picha hii kwa hatua zaidi atakazoweza kuchukula kulingana na maoni yenu.
.end.
Subi

3 comments:

Fadhy Mtanga said...

Nami nakubali bakora ziendelee kuwepo. Lakini lazima kuwe na udhibiti.
Walimu wengi hupenda kuchapa wanafunzi bakora pasipo mipaka.
Hali hii mara nyingi huleta madhara makubwa kwa wanafunzi hao. Mi nadhani kuna haja ya mamlaka za elimu kulipa jambo hili usimamizi wa hali ya juu.

Nikiwa shule nilishuhudia uchapaji wa kikatili sana. Mwalimu moja alipenda kumshusha mwanafunzi sarawili yake na kisha kumwachia bakora pasipo huruma. Hali ile iliacha madhara makubwa kimwili na kisaikolojia kwa wanafunzi. Nakumbuka nikiwa kidato cha tatu niliingia kwenye kumi na nane za mwalimu huyo. Niligoma kufanya hivyo. Akarusha ngumi, nikaikwepa akapiga ukuta. Akasema kwa uongozi wa shule nimemtishia kumdunda. Nikasimamishwa shule miezi miwili. Kwangu ilikuwa ni afadhali hilo, hata mzazi alinielewa. Niliporudi tukaanzisha movement ya kupinga ukatili ule. Tukafanikiwa kuleta mabadiliko.

Nataka kusema kwamba, kuna walimu walio na ukatili kuliko binadamu wa kawaida anavyoweza kudhani.

Ushauri wangu kwa walimu, wabadilike. Hatukatai mtoto akikosa aadhibiwe. Lakini adhabu shurti iwe ya kibinadamu. Kiukweli toka moyoni, nawachukia mno walimu wa staili hiyo. Ningekuwa na uwezo sijui hata ningewafanyaje.

chib said...

Adhabu kwa utendaji wa kosa ni sawa, lakini isizidi ikawa ni ile ya hasira, lakini kwa binti huyu kuadhibiwa kwa kuwa kakataa kutimiza azma nyingine ya mwalimu, nashauri aende kuripoti polisi, na pia aende akatibiwe. Hakuna cha kuogopa, asipofanya hivyo huyo mwalimu ataendelea na tabia hiyo, na hatuwezi jua kama ana ukimwi. Ataangamiza maadili ya watoto na jamii. ASHITAKIWE

Subi Nukta said...

Shukrani kwa mchango wa maoni yenu. Hatua zimeshaanza kuchukuliwa kuhusiana na hili.
Shukran Fadhy na Chib!